SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / DABI YA MANCHESTER: JUMAPILI IJAYO REFA NI CLATTENBURG MAN UNITED v CITY.

   



REFA-CLATTENBURGREFA Mark Clattenburg ndie atasimamia Dabi ya Jiji la Manchester Jumapili Oktoba 25 Uwanjani Old Trafford wakati Manchester United wakiwavaa Manchester City.

Clattenburg, mwenye Miaka 40, ndie aliesimamia Dabi iliyopita Uwanjani Old Trafford wakati Man United, chini ya Meneja Louis van Gaal, ilipoinyuka City Bao 4-2 Mwezi Aprili kwa Bao za Ashley Young, Marouane Fellaini, Juan Mata na Chris Smalling.

Msimu huu, Clattenburg ameshacheza Mechi 2 za City, ambazo waliifunga Watford na nyingine kufungwa na Tottenham, na Mechi 1 ya Man United waliyoifunga Southampton 3-2.

Kwa Msimu huu, Refa huyo ameshachezesha Gemu 11 na kutoa Kadi za Njano 11 na Kadi Nyekundu 2.

Timu hizi zinatinga kwenye Dabi hii zikitoka kwenye ushindi wa kishindo wakati Man United wakiitandika Everton 3-0 huko kwao Goodison Park na City kuiwasha Bournemouth Bao 5-1 huku wakicheza bila ya Mastaa wao Majeruhi, Sergio Aguero na David Silva, ambao pia wataikosa Dabi hii.

MANCHESTER-DERBY
Kwenye Msimamo wa Ligi, City wako kileleni wakiwa Pointi 2 mbele ya Man United ambao wako Nafasi ya 3 wakilingana na Timu ya Pili Arsenal kwa Pointi ila Arsenal wako juu yao kwa ubora wa Magoli.

Tayari Van Gaal ameshaipigia la mgambo Dabi hii kwa kusisitiza ushindi kwa Man United utatoa mkazo kuwa wao wapo rasmi kwenye mbio za Ubingwa Msimu huu.
MAREFA-OKT25
 LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumatatu Oktoba 19
2200 Swansea v Stoke
Jumamosi Oktoba 24
1700 Aston Villa v Swansea            
1700 Leicester v Crystal Palace               
1700 Norwich v West Brom             
1700 Stoke v Watford            
1700 West Ham v Chelsea     
1930 Arsenal v Everton         
Jumapili Oktoba 25
1500 Sunderland v Newcastle                  
1705 Bournemouth v Tottenham              
1705 Man United v Man City           
1915 Liverpool v Southampton              

       

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply