SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / HALI YA NSA JOB SI NZURI, VIPIMO VYAONYESHA FUVU LAKE LIMEATHIRIKA VIBAYA



PICHA YA KIPIMO CHA CT SCAN KINACHOONYESHA FUVU LAKE LIMEATHIRIKA
Uchunguzi wa mwanzo wa madaktari katika Hospitali ya KCMC mjini Moshi, unaonyesha Nsa Job ameumia sana.

Rafiki yake wa karibu ameiambia blog hiii kwamba bado hali ya kiungo huyo mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Coastal Union si nzuri.

“Walifanya kipimo cha CT Scan kuangalia kuhusiana na fuvu lake. Inaonekana limeumia sana kwa kweli na hali yake si nzuri,” alisema rafiki huyo.

 
NSA (KULIA) WAKATI AKIITUMIKIA YANGA

Nsa alipigwa jiwe kubwa juzi usiku karibu na nyumba na Davis Mosha ambaye ni mgombea wa ubunge Moshi Mjini kupitia CCM.

Alikuwa akitokea kwa Mosha ambaye ni rafiki yake, watu wanaosadikiwa ni wafuasi wa Ukawa ndiyo walipiga jiwe lililopasua kioo cha gari alilokuwamo na kumjeruhi vibaya.

Jana Mosha aliiambia blog hii kwamba wakati anakwenda nyumbani kwake alikuta watu hao wakiwa wameziba barabara na mawe makubwa.

Aliwasihi kuacha vurugu akisisitiza si jambo la busara, wakamsikiliza.


Lakini baadaye wakaanza kuwashambulia karibu kila mmoja aliyekuwa akipita katika barabara hiyo kwenda au kutoka kwake.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply