STAA wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ametoboa siri
ya kujichora tattoo yenye jina la mpenzi wake Naftari Mlawa ‘Nuh’
akisema alifanya hivyo ili kumpa imani mwanaume huyo kuwa anampenda
sana.
Akizungumza na gazeti hili juzikati, Shilole alisema siku zote mpenzi
wake hakuwa akiamini kama anampenda, licha ya ukweli kwamba naye alikuwa
amechora tattoo yenye jina lake.
“Nuh alikuwa haamini kama kweli nina mapenzi ya dhati kwake, niliamua
kuchora tattoo ya jina lake na sasa ameamini nampenda, mapenzi yetu
yameimarika kuliko mwanzoni, amejiona ni mtu muhimu sana kwangu, kwani
hata mwanaume yeyote akiona nimejichora jina hili, lazima ashtuke na
aone kwamba nina mtu tunayependana,” alisema.
Tagged with: BURUDANI
Hakuna maoni :