Mkazi
wa Arusha na mpenzi wa bia ya Serengeti Premium Lager Laota Elias
akishiriki katika shindano la mwisho la kumtafuta Serengeti Masta wa
jumla kwa mkoa wa Arusha katika kuitambua ladha halisi ya bia ya
Serengeti Premium Lager. Mashindano hayo ya mwisho yalifanyika katika
baa ya Bondeni iliyopo Kijenge juu jijini Arusha ambapo yaliwakutanisha
washindi mbalimbali wa baa za mkoa huo waliofika kuchuana vikali ili
kumpata mshindi wa jumla. Kampeni hiyo imefikia tamati jijini humo baada
ya kudumu kwa takribani miezi miwili ikizunguka baa kwa baa kusaka
washindi waliopewa jina la “Serengeti Masta”.
Mkazi
wa Arusha Cleophas John akifurahi pamoja na marafiki zake baada ya
kupita kwenye ngazi ya kwanza ya shindano la kumtafuta “Serengeti Masta”
wa mkoa wa Arusha linaloendeshwa na bia ya Serengeti Premium Lager toka
SBL wakati wa shindano
hilo ambalo lilifanyika katika baa ya Bondeni-Kijenge juu jijini
Arusha. Shindano hilo limefikia tamati jijini humo baada ya kudumu kwa
takriban miezi miwili (2) ikiwaburudisha na kuwazawadia wateja wa bia
hiyo na kuwafundisha wahudumu wa baa mbalimbali juu ya utoaji huduma kwa
wateja
Mratibu
wa mashindano ya kumsaka Serengeti Masta Yassin Khalfan (katikati)
akiwa na baadhi ya washiriki wa shindano hilo kutoka Baa mbalimbali
jijini Mbeya kushoto ni Faraji Mbwambo kutoka Gambino Bar na Ibrahim
Allan kutoka Liz Pub. Kampeni
hiyo ya Serengeti Masta imewakutanisha wateja na mameneja wa bia hiyo
katika kujifunza kwa undani kuhusiana na bia ya Serengeti Premium Lager
ambapo mameneja hao walitoa zawadi mbalimbali kwa washindi walioweza
kuitambua ladha halisi ya bia hiyo katika kipindi chote cha kampeni
ambapo pia waliweza kuwafikia wahudumu wa baa zaidi ya 4000 katika miji tofauti.
Mshiriki
wa shindano la Serengeti Masta na mkazi wa Arusha Daniel Mwakasungule
akionja ladha tofauti za bia zilizo mbele ya meza yake ili kuitambua
ladha halisi ya bia ya Serengeti Premium Lager katika shindano la
kumpata Serengeti Masta wa mkoa wa Arusha ambalo lilifanyika katika Baa
ya Bondeni, Kijenge juu jijini Arusha mwishoni mwa wiki hii.
Mshindi
wa jumla wa shindano Serengeti Masta kwa jiji la Mbeya Faraji Mbwambo
kutoka baa ya Gambino jijini Mbeya akionesha kitita cha fedha sh.
100,000 alizotunukiwa baada kuibuka mshindi wa jumla wa kuitambua ladha
ya bia ya Serengeti Premium Lager kati ya vinywaji vitano
vinavyozalishwa na kampuni ya SBL. Kampeni
hiyo ya Serengeti Masta imewakutanisha wateja na mameneja wa bia hiyo
katika kujifunza kwa undani kuhusiana na bia hiyo ambapo mameneja hao
walitoa zawadi mbalimbali kwa washindi walioweza kuitambua ladha halisi
ya bia hiyo katika kipindi cha kampeni
Mmoja wa wateja na mnywaji maarufu wa bia ya Serengeti Premium Lager Tuntufye Mwakaje maarufu kwa jina la “Tupac” akiburudika na bia hiyo wakati wa shindano la kumsaka Serengeti Masta wa jumla kwa wakazi wa jiji la Mbeya lililofanyika kwenye baa ya Mbeya Pazuri.
Hakuna maoni :