SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / HAYA NDIYO MALENGO YA SAMATTA ATAKAPOKWENDA ULAYA




TP Mazembe ipo katika harakati za kumuuza straika Mbwana Samatta kwenda Lille ya Ufaransa, lakini meneja wa mchezaji huyo, Jamal Kasongo ametoa sharti jipya la nyota huyo kwa timu atakayoenda.



Kirahisi tu, Kasongo amesema Samatta ni lazima ajiunge na timu yenye uwezo wa kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya (Uefa) au Kombe la Europa, ambako anaweza kukutana na Wayne Rooney wa Manchester United au Santi Cazorla wa Arsenal.

Kasongo alisema mpaka sasa wana ofa kutoka timu za mataifa matano lakini jambo la msingi kwao ni kuangalia uwezekano wa kucheza katika klabu inayoshiriki michuano mikubwa Ulaya.

“Bado tupo katika mazungumzo kwa sababu ofa ambazo mpaka sasa tunazo mezani zinatoka katika nchi za Ujerumani, Ufaransa, Bulgaria, Hispania na Ubelgiji, ila ukiitoa Bulgaria, nchi zilizobaki anaweza kucheza.
“Hatuwezi kusema moja kwa moja kama anakwenda Ufaransa kwa sababu tunataka timu ambayo itacheza michuano hiyo ya Uefa na pia iliyo katika hali nzuri kwa masuala ya maslahi.

“Samatta akicheza Uefa au Europa atakuwa amefika mbali sana na atajitangaza yeye mwenyewe na Tanzania kwa jumla hivyo ni lazima tuliangalie hilo kwanza,” alisema Kasongo.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply