SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

BURUDANI

Kwa hili linalotokea kwa Diamond kwa sasa ni kama kero kwa baadhi ya watu lakini ni sherehe kwa upande wa mashabiki wake kutokana na kila siku anaibuka na stori mpya na kubwa ambazo zinateka vichwa vya habari.

Baada ya hapo jana stori ya kumpatia zawadi ya gari Raymond kukiki, leo yameibuka mapya na makubwa zaidi baada ya hitmaker huyo wa Kidogo kuonekana akiwa na staa wa Nigeria, Wizkid huku mashabiki wakijiuliza nini kinaendelea?

Vipande viwili vya video alivyopost Diamond kwenye mtandao wake wa Instagram akiwa na staa huyo wa Nigeria vimewashtua mashabiki kutokana na hitmaker huyo wa ‘Shaba’ kwa sasa siyo msanii wa kitoto kwa kuwa muziki wake tayari tayari umepenya nchini Marekani na tayari ameshafanikiwa kufanya collabo na mastaa wa nchi hiyo akiwemo Swizz Beat, Drake na Chris Brown.


Haikuwa ngumu kwa hitmaker wa ‘Kidogo’ kukutana na staa huyo kutokana tayari wameshakutana mara kadhaa ikiwa ni pamoja na kufanya show kwenye jukwaa moja ikiwemo ile ya ‘One Africa’ iliyofanyika nchini Marekani mwezi uliopita pamoja na ile iliyofanyika nchini mwaka jana kwenye viwanja vya Leaders Club.

Hata hivyo inadaiwa kuwa vipande hivyo vya video vinavyowaonyesha wasanii hao walikutana Afrika Kusini na siyo Bongo kama watu wanavyofikiria kwakuwa huenda Wizkid aliondoka Dar August 22.
Mr Blue amekiri kuwa skendo yake kuwa amekuwa akiwasiliana na ex wake, Naj ambaye kwa sasa ana uhusiano na Barakah Da Prince ilitaka kuivunja ndoa yake.

Akiongea na Clouds FM, rapper huyo wa ‘Mboga Saba’ amedai kuwa mke wake, Wahyda sasa amekuwa na wivu wa kufa mtu tangu kuzuke skendo hiyo.

“Sasa hivi naona kama wivu umezidi baada ya hii skendo ya hawa jamaa kuitengenezea kiki kwasababu wanataka kutoa nyimbo yao, skendo kwamba mimi nilimpigia yule mwanamke mwingine nani anaitwa, Najma yule. Wametengeneza kweli kabisa, mimi nimezipata za kunyapianyapia kwamba wametengeneza ili kukikisha nyimbo zao,” amesema Blue.
“Lakini wamenikosea sana kwasababu wanataka kugombanisha ndoa yangu, mimi nina mke ujue, siwezi kumpigia mtu ambaye nimemwacha, ni kosa kubwa sana, halafu mke wangu yule ni mwanamke ambaye walikuwa watatu kupigania nani awe na mimi, yaani bora hata ningempigia mtu mwingine,” amesisitiza.

“Ilifika karibu kama siku mbili tuna ugomvi mimi na mke wangu, ni kitu kikubwa sana, nimekasirika sana, nimechukia sana na nawaambia mashabiki wangu, alichokifanya Barakah na watu wake, kama sio yeye simlaumu, kama watu wake nilikuwa naomba waoneshe proof kwenye mitandao waoneshe namba yangu niliyompigia, waioneshe kwamba ni hiyo kweli sio unaongeaongea tu.”
Baada ya ukimya wa muda mrefu sana wa wakongwe wa muziki wa Bongo Flava story zilizopo mtaani ni kuwa Ferooz ni miongoni mwa wasanii wanaotumia madawa ya kulevya na ndiyo sababu iliyompoteza kwenye reli ya muziki.

Kupitia Enewz Ferooz alikanusha tuhuma hizo na kudai kuwa misongo ya mawazo ndo huwa inawapelekea wasanii kuingia katika matumizi hayo ya madawa ya kulevya na kuwataka wengine wasifanye hivyo.

Ferooz amesema kuwa “Ni mara kumi upate UKIMWI kuliko uwe unatumia madawa ya kulevya” lakini pia akaongezea kwakusema “Nawashauri watu wengine pamoja na wasanii wenzangu wasije wakajaribu kufanya hivyo”.
Kazi ipo! Video Queen asiyeishiwa vituko Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ anadaiwa kuopoa kigogo ambaye ni mfanyabiashara wa madini, mkazi wa jijini Arusha ambaye ndiye mwandani wake anayempa jeuri kwa sasa.

‘Ubuyu’ kutoka kwa chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu wa mwanadada huyo unatonya kuwa, licha ya ‘umapepe’ wa Gigy ambaye kwa sasa safari za Dar na Arusha hazikauki, ukweli ni kwamba jamaa huyo hapindui kwake.

Ili kupata mzani wa ubuyu huo, Over Ze Weekend lilimsaka Gigy, alipopatikana kwa njia ya kilongalonga alikiri kuwa na kigogo huyo na kudai kwamba wameshibana sana.
Msanii wa nyimbo za injili nchini, Rose Mhando, ameshtakiwa kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye, kwa kitendo cha utapeli na kushindwa kutekeleza mkataba wa kuhudhuria na kutumbuiza kwenye Tamasha la Pasaka lililofanyika jijini Mwanza licha ya kulipwa gharama zote alizotaka.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions inayoongozwa na Alex Msama, ambayo ina mkataba naye imekuwa ikiuza na kuandaa matamasha ya msanii huyo pamoja na tamasha la Pasaka la kila mwaka, alimweleza Waziri Nnauye, mbele ya halaiki ya wananchi alipokuwa mgeni rasmi wa sherehe za tamasha hilo lililofanyika kwa mara ya kwanza jijini Mwanza na mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Msama alieleza kusikitishwa na kitendo cha Rose Mhando kuingia mitini ilihali akiwa ameingia mkataba na kulipwa gharama zote pamoja na nauli alizodai kabla ya kuanza safari kufika Geita, Mwanza na Kahama kujiunga na wasanii wenzake kwa ajili ya kutumbuiza katika tamasha hilo.

“Mheshimiwa Waziri, Rose Mhando naye amekuwa ni jipu kwa kuwa amefanya utapeli kwa kukubali kulipwa gharama zake zote lakini ameshindwa kuhudhuria na kutumbuiza kama wenzake wakina Solomon Mkubwa, Bonny Mwaitege, Upendo Nkone na wengine uliowashuhudia hapa.

“Hii ni mara ya tatu amekuwa akifanya hivi na mara kwa mara nimekuwa nikimsamehe,” alisema bila kutaja kiasi alichomlipa katika mkataba waliokubaliana ili aweze kufanya onyesho hilo.

Msama pia akatumia fursa hiyo kuwaomba radhi wananchi waliofika katika Uwanja wa CCM Kirumba kwa kutegemea mwimbaji huyo angekuwepo na kutumbuiza na wenzake lakini kilichotokea ni aibu na utapeli wa msanii huyo mkubwa wa nyimbo za injili aliyejizolea umaarufu ndani na nje ya nchi.

“Kuanzia leo mtu yeyote asije akaingizwa mjini na Rose Mhando kwa kuingia naye makubaliano akidhani yupo chini ya Kampuni ya Msama Promotions, kwa kitendo alichoendelea kukifanya naomba kutangaza rasmi kuvunja mkataba wa kufanya kazi na msanii huyo ili kulinda hadhi na heshima ya Kampuni yangu,” alisisitiza Msama.

Msama aliomba wananchi waendelee kuipa sapoti kampuni yake kwa kuwa imekuwa ikirejesha mapato ya viingilio na sadaka katika tamasha hilo kwa jamii hasa kwa watu wasiojiweza, makundi maalumu pamoja na kuendeleza vipaji vya wasanii chipukizi wa nyimbo za injili nchini kote.

Hata hivyo, wadau mbalimbali waliokuwepo katika uzinduzi huo walisikitishwa na kutokutokea kwa mwanamuziki huyo huku wengine wakimlalamikia kuwa na tabia hizo kwa muda mrefu na kufanya bila woga na hofu yoyote.

Mwanamuziki huyo aliwahi kuripotiwa kutuhumiwa kufanya udanganyifu kwa kupokea zaidi ya Sh milioni 3 na kisha kushindwa kufanya onyesho katika tamasha la nyimbo za injili lililoandaliwa mkoani Njombe mwaka jana.

Mkurugenzi wa Kampuni ya The Comfort Gospel Promotions, Seth Sedekia, ndiye alimfungulia kesi hiyo  katika kituo kikuu cha polisi Njombe na akapewa RB namba: NJ/RB/1793/2015.

Kushindwa kutokea kwa mwanamuziki huyo siku hiyo ya Jumapili iliyopita, kuliwafanya mashabiki waliokuwa wamelipa kiingilio cha shilingi 5,000 kila mmoja kuzusha vurugu kubwa kwa mwandaaji huyo wakidai wametapeliwa huku wengine wakionyesha kuchukizwa na kitendo cha mwanamuziki huyo kushindwa kutokea kufanya onyesho hilo.

Mwandaaji wa onyesho hilo, Sedekia alisema amefikia hatua ya kufungua kesi kituo cha polisi kufuatia kumlipa fedha zote shilingi milioni tatu Mhando ambazo alisaini mkataba naye akiwa mjini Dodoma kwa ajili ya kufanya onyesho mjini Njombe. Katika onyesho hilo, Mhando alitarajiwa kushirikiana na msanii wa nyimbo za injili, Happy Kamili kutoka jijini Mbeya ambaye alifika katika tamasha hilo akishirikiana na wasanii wengine kutoka mjini Njombe.

Ofisa Habari wa Kamanda wa Polisi mkoani Njombe, Franco Malimba, alipoulizwa juu ya kuwepo kwa taarifa hizo katika kituo cha polisi, alikiri kuwepo lakini alisema hawezi kulizungumzia kwa sababu halijafika ngazi za juu.
Jux ameweka wazi hisia zake hizo baada ya kufanyiwa mahojiano na eNewz ambapo alisema kuwa yeye pia ni mwanamuziki kama ilivyo kwa Vanessa Mdee na kusema kuwa imejengeka kuwa kila interview anayoifanya ni lazima watu wamuulize kuhusu uhusiano wake na Vanessa na kwasasa imeibuka ya kumuuliza juu ya Jack Cliff.

Jux alishawahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na ‘video vixen’ Jack Cliff ambaye anashikiliwa nchini China kwa kukutwa na madawa ya kulevya na kwasasa staa huyo anajihusisha na mahusiano ya kimapenzi na mwanamuziki mwenzake Vanessa Mdee.

Jux anasema kuwa kuna mambo mengi sana ya kuzungumza kwenye interview ambayo yatakuza muziki wake mbali ya kuzungumza mambo ambayo yatakuwa hayasaidii mahusiano yake wala muziki wake.


WIFE....Honey plz lets come and help
me in the garden to clean these
flowers??
MME.......Are you mad ,do I look like a
gardener?
WIFE.....Ok sory babie,...but
sweetheart please go and fix that
door to the bathroom,Junior broke it
last night??
MME.....I hate your nosense
requests,,do I look like a Carpenter??
..
At night MME came back from town
and found that the garden is clean
and the door if fixed well..he was
surprised and decided to ask his wife..
..
MME.....Honey I can see the garden is
clean and the Door is well fixed,who
fixed the door for you??
WIFE.....Its our neighbour ofcourse..
MME.....Woow thats great,,did he fixed
it for you free of charge?
WIFE........NO he gave me two options
to choose,,,He said I must give him
BREAD OR SE..X..
MME.....I hope you gave him BREAD??
WIFE....What???....Do I look like
BAKERY???
Video Queen na msanii wa filamu Bongo, Gift Stanford ‘Gigy
Money’ ameweka wazi kuwa yupo tayari kucheza picha za ngono endapo atapata mshiko wa maana.

Akistorisha na gazeti hili wikiendi iliyopita, Gigy alisema kwa kuwa anatafuta fedha ya kubadili maisha yake, anaweza kufanya tendo hilo kwa sababu anahitaji kuishi kitajiri zaidi.

Aliendelea kusema kuwa amewahi kufuatwa na watu mbalimbali kutoka Dubai wakimtaka kwenda kucheza filamu hizo, lakini alikataa kutokana na fedha walizomtajia kuwa ni kidogo na hakuwa tayari kwa muda huo.


“Yaani nikiambiwa napewa mamilioni nicheze picha hizo nipo tayari maana hapa duniani wanaokula starehe zaidi ni wale wenye fedha sasa nikipewa mamilioni ili nibadili maisha yangu, niko tayari maana nitabadili maisha yangu na nitaishi kitajiri hapo mpaka watu waje kunishtukia nitakuwa nimeshakula bata vya kutosha,” alisema Gigy.

Gigy Money ni miongoni mwa ma-video Queen chipukizi wanaofanya vizuri katika video za wasanii wa muziki wa kizazi kipya.

Chanzo:GPL

1. Mama mwenye mtoto/watoto aliyeachika akiwa kwenye ndoa

2. Mwanamke aliyeachika ndani ya ndoa

3. Mwanamke yupo karibu mitandao yote ya kijamii, hakuna habari ya kimbea yeye anapitwa (Tena siku hizi WhatsApp wanawake hasa akina dada wana magroup, hadi migegedo ya saizi mbalimbali wanatumiana)

4. Mdada aliyeenda umri halafu anaishi gheto ( Hawa mara nyingi wamekubuhu, hadi wanaume wakwere wanawakwepa, wadada hawa hujifanya social, wana msururu wa marafiki wa kiume, mara nyingi hit and run kwao ni kawaida)

5. Mdada unayemtongoza siku moja, ya pili au ya tatu ukimwita kwako, anajileta. Kumbuka wewe sio wa kwanza kumtongoza, wewe labda ni wa hamsini.

Mtangazaji mahiri wa kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM Millard Ayo baada ya kufungua studio yake kubwa naya kisasa jijini Dar, ameanza kuuza vipindi vya burudani katika radio mbalimbali za Afrika Mashariki.


Akizungumza Jumamosi hii katika mdahalo wa kuwatia moyo wanafunzi waliofeli kidato cha nne, ambao ulienda sambamba na uzinduzi wa video mpya ya Mrisho Mpoto, Millard alieleza mafanikio yake baada ya kupambana kwa muda mrefu.

“Nilijiuliza kwanini nisitumie uandishi wangu wa habari ili kusambaza habari Afrika?, ndipo nikaanza kujinyima ili nijenge studio yangu kwa pesa yangu mpaka imekamilika. Sasa hivi tayari nimeshaanza kuuza vipindi vyangu katika radio mbalimbali za Afrika, Kenya, Rwanda. Pia nimekuwa reporter wa radio mbalimbali za Afrika Mashariki, pia Nigeria kuna kazi maalum nimepata ambayo nimehifurahia sana,” alisema Millard.

Aliongeza, “Nimeona kama Rwanda na Kenya sasa hivi bongofleva ndiyo imetake over, hawa watu ingawa wanasikiliza muziki, pia wanataka stori mbalimbali za mastaa wa bongofleva. Kwa hiyo mimi nataka kuwaambia watu wangu tusikate tamaa kama ulianguka inuka endelea,”

Pia Millard Ayo alisema yeye ni miongoni mwa wanafunzi ambao walifeli kidato cha nne lakini aliinuka na kuendelea.

Usiku wa March 5 2016 nyota ya Tanzania iliweza kushine vilivyo kunako tasnia ya uigizaji baada ya waigizaji wa Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Single Mtambalike ‘Rich Richie’ kunyakua Tuzo za (MVCA) zilizofanyika jijini Lagos nchini Nigeria. Tuzo hizo pia ziliweza kuhudhuriwa na mastaa wengi tu wa kibongo.
LULU



Watanzania watakuwa sehemu ya wale watakaoshiriki katika tuzo maarufu za African Magic Peoples Choice Awards.

Tuzo hizo zinatarajia kufanyika kesho jijini Lagos nchini Nigeria na Watanzania wasanii wa filamu wamepata nafasi.

Msanii mkongwe wa filamu nchini Richie Richie, yeye amefanikiwa kuingia kwenye vipengele viwili vya Best East African na Best Swahili kupitia filamu ya Kitendawili.



HONEYMOON

Mwanadada Honeymoon Mohammed ambaye ni muongozaji ameingia katika kipengele cha East African kupitia filamu yake ya DADDY’S WEDDING.



Wengine ni Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ambaye anaingia katika kipengele cha East African pia, Ameir Shivji katika kipingelea cha Best Swahili kupitia filamu ya Samaki Mchangani huku Mtanzania mwingine akiingia kwenye kipengele cha East African kupitia filamu ya Mpanngo Mbaya.

Msanii wa filamu nchini na aliyekuwa akitoka kimapenzi na msanii Nay wa Mitego amefunguka na kusema kuwa bado aliyekuwa mgombea wa urais nchini mwaka jana.

kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo yupo moyoni mwake.
Kupitia Account yake ya Instgram Shamsa Ford alipost picha ya Mh Edward Lowassa na kusema ni kumbukumbu yake lakini siku zote atakuwa na nafasi moyoni mwake.

"My FIRST TBT...YOU will always have a space in my heart dady...✌✌" Aliandika Shamsa Ford
Kipindi cha kampeni za uchaguzi Shamsa Ford alikuwa ni kati ya wasanii ambao walionyesha wazi kumpa support Mgombea wa urais kwa tiketi ya CHADEMA na aliyekuwa akiungwa mkono na UKAWA, Mh Edward Lowassa.

Lakini kutokana na post hiyo wapo baadhi ya mashabiki ambao walionyesha kutopenda ujumbe wake huo huku wengine wakimuunga mkono kwa kusema kuwa Edward Lowassa alistahili kuwa kiongozi wa juu wa nchi, kama ambayo Comment zinavyosema hapo chini.
"Miaka elfu moja haitatokea awe Rais labda awe Rais wako wewe Shamsa na Nay mibangi wako" Peterteddy31

"Huyo hatumtaki sasa hivi hapa ni kutumbua mijipu tu mabadiliko peleka Monduli maana tulichotaka tunakiona kwa Magufuli wewe huna jipya" Alisema Saidi_geleta
"Huyo ndio Mr president wangu hata wanune ukweli wanaujuaaa u winn" Alisema mc_nyemolicious
"Hapo nakupendaga sana Shamsa Ford, ni vizuri kuamini unachoamini ni sawa, na ni mbaya kumdhihaki mtu anachoamim" Alisema frankatilio
Ewe mwanaume ukioa mwanamke:

Mrefu, jua kwamba utaoa mwanamke mpenda maendeleo, mchapa kazi na mkarimu ila hawajui mapenzi na ni wavivu kujiweka safi kimazingira.

Mfupi kiasi, jua ya kwamba utaoa mwanamke mchangamfu na mpenda elimu sana ila tu wanapenda mnongono na hawaridhiki.

Mfupi kabisa.Jua ya kwamba utaoa mwanamke msikivu na mcha Mungu ila ni waroho kwa kula na wabishi sana.

Ewe mwanamke ukiolewa na mwanaume:

Mrefu, jua ya kwamba utaolewa na mwanaume mwenye upendo, utu na ubinadamu ila ni wabahili mno na hawapendi kupendeza.

Mfupi kiasi, jua ya kwamba utaolewa na mwanaume mwenye fikra na akili timamu za maendeleo, mbunifu, mcheshi na fundi wa mahaba ila ni wapenda ushirikina sana, wana wivu na wambea sana na mara nyingi hupenda kupiga chabo kwa watu wanaofanya mapenzi.

Mfupi kabisa, jua ya kwamba utaolewa na mwanaume mwaminifu, msikivu, mnyenyekevu ila huwa wepesi wa kujiua, kukata tamaa upesi, wanawivu sana na hawapendi kuoga.
Nawatakieni kila la kheri wale wenye wapenzi na ambao mnajiandaa kuoa au kuoelewa ila zingatia sana tabia hizo hapo juu za huyo unayetegemea kufunga nae pingu za maisha ili usije kutusumbua baadae. Chukueni tahadhari!
Siku moja baada ya mastar wakubwa Kim Kardashian na Kanye West kupost picha ya mtoto wao wa pili aitwaye ‘Saint West’ ameonesha kumchanganya sana bidada Wema Sepetu kwa kile alichokifanya kwenye mitandao yake ya kijamii.


Wema Sepetu jana amepost picha zaidi ya tatu Instgram za mtoto huyo huku akionesha ni jinsi gani ametokea kumpenda mtoto huyo na kudai ni mzuri sana, lakini haikuishia hapo Wema Sepetu aliamua kuweka picha hiyo kwenye Profile yake Instgram na kuweka picha hiyo kama Wall Paper na Screen save kwenye simu yake.

“Gnyt now… But Kimberly Kardashian sio kwa mtoto mzuri hivi jamani. Kama Pipi…!!! Mashallah jamani… God…! You are Able…! Saint West mzuri mno jamani… Dis Baby Boy too pretty ooo” Aliandika Wema Sepetu.

Kutokana na kitendo hicho mashabiki wa Wema ambao wanafahamika kama Team Wema walianza kumfariji Wema na kumpa maneno yenye faraja na yenye kumtia moyo kuwa ipo siku na yeye atapata mtoto, kwani Mungu ndiye anapanga kila jambo.

“Mungu hutoa kwa wakati wake na kwa sababu zake. Kama alivyowaona wengine na wewe atakuona hivyohivyo. Naatakupa haja ya moyo wako. Mungu tu ndio atakae weza kukusaidia my dear wema. Worry out your time will come soon keep on hoping that I love u.” Aliandika Hoperitha Minja

“Usijali iposiku utakuja kuzaa na mwanaume wa furaha yako ulio mpenda na yeye akakupenda, ninavyo kupenda kama mtanzania mwenzako kilasiku nakuombea kwa Mungu akupe afya na maisha marefu uzidi kututungia kazi nzuri na zitambulike dunia nzima I love you Wema” Aliandika king._of_ma_love_davi

Ingawa si watu wote walipendezwa na maneno ya Wema Sepetu kumsifia mtoto huyo ndipo hapo aliwaamsha watu ambao wamezoea kumtolea maneno machafu na wanaotumia lugha chafu na za kuudhi si kwake tu bali hata kwa watu waliostaarabika na watu wenye utu, kwani wasingweza kutumia maneno ambayo wanajua wazi yanaweza kuumiza wengine.

Rapper mkongwe kwenye tasnia ya muziki nchini Tanzania, A.Y amefunguka na kusema kuwa bado hajapata msukumo wowote wa kuoa toka nafsini mwake.

Rapper huyo aliyasema hayo kwenye mahojiano yake na kituo kimoja cha Tv na kuongeza kuwa ndoa ni wito,ukimwita ataitika

“Ndoa ni wito kuna sauti huwa inakwambia kabisa huu ndio muda wako,sauti hiyo kila nikiiita nasikia mwangwi tu” alisema A.Y na kutania kuwa mpaka swahiba wake Mwana Fa aoe kwanza maana yeye ndio mkubwa

Baada ya Ray Kigosi kuweka wazi kuwa anakunywa sana maji ndio maana anakuwa mweupe, Godzilla pamoja na mashabiki mbalimbali katika mitandao ya kijamii wamenza kufanya zoezi hilo kwa kuwahamasisha watu kunywa maji ili na wao wapate upako huo.

Hivi karibuni Ray Kigosi kupitia kipindi cha Enewz cha East Africa Television alidai kuwa weupe wake una sababishwa na kunywa maji ya kutosha pamoja na kufanya mazoezi.

Msanii Afande Sele ambaye anawakilisha mkoa wa Morogoro katika muziki amefunguka na kusema kuwa hataki kuja kuwa binadamu tena bali anahitaji kuwa Malaika.

Afande Selle alisema hayo kupitia kipindi cha Planet bongo cha East Africa Radio na kusisitiza kuwa siku atakayo kufa anaomba achomwe moto kwani yeye anaamini katika moto na si kuzikwa kawaida.
Afande Sele alidai kuwa amechoka kuwa binadamu bali anataka kuwa Malaika ndio maana anahitaji kuchomwa moto ili siku ya ufufuo arudi kama Malaika na si binadamu, imani yake inamtuma kuwa akizikwa kwenye udongo siku ya ufufuo atarudi kuwa binadamu tena jambo ambalo yeye hataki kusilisikia tena.

Kufuatia imani hiyo Afande Sele amesema mpaka sasa ameacha wosia kuwa siku atakayokufa achomwe moto na si kuzikwa.

Idriss na Wema Sepetu
Zikiwa zimepita siku kadhaa toka Idris Sultan kuweka wazi kumpa ujauzito bidada Wema Sepetu kupitia katika account yake ya Instagram Wema Sepetu amefunguka na kusema kuwa Idris amempa heshima na kumfanya ajivunie kuwa mwanamke.

Wema Sepetu leo kupitia ukurasa wake wa Instgram amefunguka mambo mengi na kuonyesha kufurahishwa na wala hajutii kuanzisha mahusiano na Idris Sultan, katika ujumbe wa Wema anasema wazi anampenda Idris si kwa sababu tu na yeye anampenda hapana bali ni kutokana na ukweli kwamba Idris ametengeneza historia nyingine katika maisha yake na kumfanya kuwa mtu bora na kubadili kabisa maisha yake.

Wema Sepetu alizidi kushusha shukrani kwa kijana huyo na kusema ikiwa leo ni siku yake ya kuzaliwa Idris Sultan anataka kumueleza kuwa yeye Wema Sepetu anajiona ni mtu mwenye bahati kumpata yeye kama mtu wake au mpenzi wake na kusema atamtunza na kumheshima kwa muda mrefu sana.

Zifuatazo ni baadhi ya nukuu kutoka kwa Wema Sepetu katika ujumbe wake huo ambao umekuwa ujumbe maalumu kwa mpenzi wake huyo katika siku yake ya kuzaliwa.

" Nimeandika na kufuta karibia mara mia maana kila ninachotaka kuandika najikuta naona hakifai and maybe hakitoshi.... Im busy looking for the Proper words to tell you how I truly feel but naona kama sio.... I thought deep and I jus simply decided to write this Idris I love you, not only because you are my man or because you love me too No...!!! I love you because you make me a Better person, You changed my whole life.... You Complete me" Alisema Wema

"You are the only person That has really made me feel like a woman.... Oh...! I just love you with all my heart... Now before The Clock strikes 12, Let me be The 1st to wish you a Happy Birthday My Love " Alimaliza Wema Sepetu

 Leo ni Siku ya Kuzaliwa kwa Mchumba mpya wa Wema Sepetu Idriss Sultan Mshindi wa Big Brother Mwaka juzi...Pichani Wema Sepetu Akimpongeza kwa kwa kuonyesha mahaba mazito