SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

MICHEZO


Manchester City (4-2-3-1): Hart 7, Maffeo 6.5, Stones 7 (Adarabioyo 60, 6), Kolarov 6.5, Clichy 6, Toure 7, Fernando 6, Delph 6.5, Jesus Navas 6, Iheanacho 7.5 (Fernandinho 76), Nolito 6 (Tasende 60, 6)
Subs: Gunn, Sterling, Aguero, Silva
Goals: Delph 56 
Steaua Bucharest (4-5-1): Cojocaru 6.5; Aganovic 6 (Stanciu 53 6.5), Tamas 6.5, Mitrea 6.5, Momcilovic 6; Enache 6, Sulley 6 (Achim 62 6), Bourceano 7, O Popescu 6 (Popa 53 6), Hamroun 6; Tudorie 6
Subs not used: Nita, Simion, Valceanu, D Popescu 
Man of the match: Iheanacho 
Referee: Pawel Gil 6 (Poland)
*Ratings by Joe Bernstein at the Etihad Stadium 








SALVATORY EDWARD
Kiungo wa zamani wa timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Ngawina Ngawina, pamoja na kiungo wa zamani wa Yanga, Salvatory Edward wameanzisha kituo cha kuibua vipaji vya wanasoka chipukizi chini ya umri wa miaka 17 na kuviendeleza.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ngawina alisema kituo chao kinaitwa Kambiasso Sports na kwamba kwa kuanzia Jumamosi wiki hii watafanya kliniki maalum ya kusaka vipaji hivyo kwenye Uwanja wa Tandika Mabatini, Dar es Salaam, dhamira yao kubwa ikiwa ni kuhakikisha wachezaji wenye vipaji wanaendelezwa na kutafutiwa timu.

“Kila mzazi mwenye mtoto ambaye anaamini ana kipaji cha soka na anahitaji aendelezwe, amlete mwanae Tandika Mabatini Jumamosi Agosti 27, ajitahidi saa mbili asubuhi awe ameshafika, kwani ndiyo muda tutakaoanza.

“Kliniki yetu itaendeshwa na makocha mahiri, ambao wana leseni za ukocha kutoka Caf (Shirikisho la Soka Afrika), ili kufanya hili jambo kiuweledi zaidi na kupata vijana wenye sifa,” alisema Ngawina.

Alisema dhamira yao ni kupata vijana wengi wenye vipaji kadri iwezekanavyo na kwamba suala la idadi itategemea na watakavyoona siku hiyo, lakini dhamira yao ni kuwa na vijana wasiopungua 30, lakini si lazima wote wapatikane Dar es Salaam, wataenda hadi mikoani.

Aliwataja watakaoendesha mshujo huo licha ya yeye na Salvatory, pia atakuwepo kocha Kennedy Mwaisabula, ambaye amepata kufundisha timu mbalimbali nchini ikiwemo Yanga.

Mwingine ni kipa wa zamani wa timu mbalimbali ikiwemo Simba ya Dar es Salaam na Ferroviario De Maputo ya Msumbiji, Muharami Mohammed ‘Shilton’, ambaye kwa sasa ni kocha wa makipa wa timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ . Pia atakuwepo kocha mwingine wa makipa Terry Muhorel.

“Soka si kama paa la nyumba kwamba siku zote linakuwa juu tu. Soka inaanzia chini na ndiko tunakotaka twende,” alisema Ngawina.

Kwa upande wake Salvatory alisema dhamira yao ni kuwa na kituo ambacho kitakuwa hazina ya nchi kwa wachezaji wa siku za usoni, lakini pia kiwe kitovu cha timu mbalimbali kuchukua wachezaji.

“Tunaamini vijana wetu wakishaiva tutawauza timu mbalimbali za ndani ya Tanzania na nje, kwani kituo kina uhusiano mzuri na watu mbalimbali waliopo hapa nchini na hata nje ya nchi,” alisema Salvatory.

 “Tunaosimamia jambo hili tumecheza mpira kwa kiasi cha kutosha, tumesomea ukocha, tunajua nini cha kufanya kuendeleza vijana wetu,” alisema.

Aliwaomba wachezaji chipukizi wa umri huo wanaoamini wana uwezo wajitokeze siku hiyo ili kuwania nafasi ya kuwepo katika kituo hicho ambacho kitakuwa Temeke, Dar es Salaam.

Baada ya kikosi cha Mwadui FC kuchapwa kwa bao 1-0 katika mechi yao ya Ligi Kuu Bara, kocha wake, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameamka na kusema, anakubali kufungwa lakini akasisitiza, walicheza mechi kwenye uwanja mbovu.

Toto African ndiyo walioichapa Mwadui FC kwa bao 1-0, katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Dar es Salaam. Shujaa wa Toto akiwa ni Waziri Junior aliyepachika bao hilo katika kipindi cha kwanza.

“Nakubali kabisa kuwa mchezo nimepoteza kwa kuwa bao lilikuwa hakuna lawama hata  kidogo. Tumepambana mwisho ukashindikana.

“Lakini uwanja tuliochezea, unaweza ni wa kuchezea ng’ombe na si binadamu. Hauna viwango na kweli umeharibika sana.

“Awali tulikuwa tucheze Jumamosi, eti mechi ikaahirishwa kwa kuwa kuna Fiesta na ajabu ligi ilishapangwa, kwa kuwa kuna shughuli ambayo si ya soka, mechi inaahirishwa,” alisema Julio.

Katika mechi hiyo, Mwadui FC walishindwa kung’ara katika kipindi cha kwanza, lakini wakacharuka katika kipindi cha pili lakini hakukuwa na mafanikio.


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeweka bayana kuwa, lipo kwenye mpango wa kuwakabidhi kombe jipya la Ngao ya Jamii timu ya Azam kutokana na kukabidhiwa kombe ambalo halikuwa lenyewe.

Azam waliichapa Yanga kwa penalti 4-1 katika mchezo wa Ngao ya Jamii baada ya kumaliza dakika tisini kwa sare ya mabao 2-2, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar. 




  Msemaji wa TFF, Alfred Lucas ameliambia Championi Jumatano kuwa, waliwapa Azam ngao ambayo siyo yenyewe kutokana na kuchelewa kukamilika kwa utengenezwaji wa ngao halali ambalo walitakiwa kupewa.

“Lile kombe ambalo tuliwapa Azam siku ile walipocheza na Yanga kwenye Ngao ya Jamii halikuwa lenyewe, bali tulilitoa kwa ajili ya kuziba nafasi ya kombe halisi ambalo lilichelewa kuja kutokana na kutokamilika mpaka inafika siku ile, hivyo tukaona siyo vizuri bingwa akiondoka mikono mitupu.

“Tumepanga kuwabadilishia na kuwapa kombe lao halisi ambalo walistahili kupewa ambalo hili litakuwa na thamani halisi na mwonekano tofauti kabisa na lile ambalo tulilitoa awali,” alisema Alfred.

SOURCE: CHAMPIONI
Kiungo wa Manchester United, Mjerumani Bastian Schweinsteiger, amesema baada ya kuondoka ndani ya kikosi hicho, hafikirii kujiunga na timu nyingine ya barani Ulaya, na badala yake ataenda kucheza soka katika Ligi ya Marekani au Asia.

Schweinsteiger ambaye amekuwa hafanyi mazoezi na kikosi cha kwanza cha United kutokana na kutokuwepo kwenye mipango ya kocha wa timu hiyo, Jose Mourinho, bado ameonyesha nia ya kuendelea kubaki klabuni hapo.

Kupitia akaunti yake ya Mtandao wa Kijamii wa Twitter, Schweinsteiger aliandika: “Manchester United itakuwa klabu yangu ya mwisho hapa Ulaya. Naziheshimu klabu zingine, lakini Manchester United ndiyo timu pekee iliyonifanya nikaihama Bayern Munich. Nipo tayari kubaki kama timu hii itaendelea kunihitaji.



 


“Hiki ndicho ninachoweza kukisema kuhusiana na hatma yangu ya sasa. Napenda kuwashukuru mashabiki kutokana na ushirikiano waliouonyesha kwangu.”

Mjerumani huyo aliyekuwa kwenye kikosi cha Ujerumani kilichotwa ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2014, mshahara wake ndani ya United ni pauni 160,000 kwa mwaka na mkataba wake umebakia miaka miwili kumalizika.


Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ametangaza kikosi cha wachezaji kikiwa na mabadiliko kadhaa ambacho atakiandaa maalumu kwa mchezo dhidi ya Nigeria.

Kikosi hicho kina wachezaji 20 ambao atasafiri nao kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo huo wa Septemba 3, 2016 lakini wachezaji wanatakiwa kuripoti kambini Agosti 28, mwaka huu na safari ya kwenda nchini Nigeria itakuwa Septemba mosi.

   


KIKOSI HICHO HIKI HAPA:
Deogratius Munish ‘Dida’
Aishi Manula
Mwinyi Haji
Andrew Vincent ‘Dante’
Juma Mahadhi
Kelvini Yondani
David Mwantika
Himid Mao
John Bocco
Farid Mussa
Jamal Mnyate
Ibrahim Ajib
Shiza Kichuya
Mzamiru Yassin
Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’
Jonas Mkude
Mbwana Samatta
 Ibrahim Rajabu
Shomari Kapombe
Simon Msuva
HANS POPPE

Ikiwa ni siku chache baada ya Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kumtaka beki Hassan Kessy kuondoa hofu kwa kuwa siku itafika atacheza, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema huenda beki huyo akaendelea kubaki nje ya uwanja kwa msimu huu na mwingine.

Manji alisema hayo juzi huku akisisitiza, Kessy hawezi kutocheza milele.

Lakini Hans Poppe amesema kinachomponza Kessy ni ujeuri wa viongozi wa Yanga ambao wanajua wamekosea, lakini wanataka kuonyesha umwamba.

Akifanya mahojiano na SALEHJEMBE jijini Dar es Salaam, Hans Poppe amesema Yanga wanajua wamefanya makosa, lakini wanataka kuonyesha umwamba kama walivyozoea.

“Waliwahi kutufanyia hivi katika suala la Yondani, safari hii wamerudia na kumsainisha Kessy wakati akiwa bado na mkataba na Simba.


“Kama hiyo haitoshi, mkataba wameufikisha TFF, wameusajili na wakatuma Caf. Sasa sisi tuna kila kitu na ushahidi mwingine wao wenyewe wameupeleka TFF na Caf.
“Kilichotakiwa ni kuandika barua, nilikutana na Chanji (kiongozi Yanga). Nikamweleza andikeni barua mimi nitalisimamia hilo. Lakini hakufanya hivyo, wanataka kuonyesha ujeuri.

“Kama itaendelea hivi, ninaamini Kessy hatacheza. Na hapa wa kulaumiwa ni wao maana Simba tupo hapa,” alisema Hans Poppe na alipoulizwa kama wakiandika barua basi mara moja watamruhusu Kessy, akajibu.


“Wakiandika barua, basi sisi tuna jibu au majibu ya kuwapa. Sasa yatapatikana kutokana na barua yao.”





MAMA MZAZI WA POGBA AMENUNUA RUNDO LA JEZI ZA MWANAYE MARA TU BAADA YA KUANZA KUINGIA MTAANI IKIWA NI SAA CHACHE BAADA YA KUJIUNGA NA MAN UNITED AKITOKEA JUVENTUS.

IMEELEZWA MAMA HUYO ANAJIANDAA KUTOA ZAWADI KWA WATU MBALIMBALI AMBAO NI WATU WAKE WA KARIBU. POGBA RAIA WA UFARANSA AMEJIUNGA NA MAN UNITED KWA KITITA CHA PAUNI MILIONI 100.



HATUA YA ROBO FAINALI YA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Kocha wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja amesema Yanga imepata jembe baada ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Coastal Union, Juma Mahadh kutokana na yeye kufahamu kiwango cha mchezaji huyo ambaye aliwahi kumfundisha kabla ya kuhamia Simba.

Mahadh ambaye ameonyesha kiwango kikubwa kwa msimu huu akiwa na Coastal Union kiasi cha kuitwa timu ya taifa, Taifa Stars, amesajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka mitatu.

Mayanja ambaye ameiongoza Simba kumaliza katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Bara amesema kuwa kutokana na kufahamu kipaji alichonacho kiungo huyo ana uhakika mkubwa ataisaidia Yanga msimu ujao.

“Mimi ndiye niliyemfanya Mahadh ajulikane kwani nilimkuta mtaani tu anacheza lakini kwa uwezo aliokuwa nao ndiyo nikamvuta Coastal Union ambapo ameonyesha uwezo wa hali ya juu mpaka sasa kusajiliwa na Yanga, jambo ambalo kwangu najisikia furaha kuona linatokea.


“Naamini kwamba Yanga wamepata mchezaji sahihi, atawasaidia sana kwa msimu ujao kwani uwezo anao na anaweza kuwapa changamoto viungo wengine

CAF-CONFED-CUP2016MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga, Leo wametumia vyema Uwanja wa Nyumba, Taifa Jijini Dar es Salaam kwakuichapa GD Sagrada Esperanca ya Angola 2-0 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mchujo ya CAF Kombe la Shirikisho.
Bao zote za Yanga, iliyocheza bila Maprfeshenali wao Donald Ngoma na Kamusoko, wenye Kifungo kutokana na Kadi za Njano, zilifungwa Kipindi cha Pili.
Bao hizo zilifungwa na Simon Msuva, Dakika ya 70 na Matheo Antony, Dakika ya 90.
Timu hizi zitarudiana huko Angola Wiki ijayo na Mshindi kutinga Hatua ya Makundi.
VIKOSI:
YANGA: Deo Munishi, Juma Abdul, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Nadir Haroub, Salum Telela [Mbuyu Twite, 46’], Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Malimi Busungu [Godfrey Mwashiuya, 53’], Amissi Tambwe, Deus Kaseke [Matheo Anthony, 77’]
GD SAGRADA ESPERANCA: Yuri Tavazes, Roadro Juan da Semero [Paul Camufingo, 64’], Dennis Conha Morais, Asenio Cabungula, Antonio da Silva Oliveira [Evanildo de Jesus Pedro, 64’], Ntaku Zabakaka, Manuel Paulo Joao, Alentua Tangala Rolli, Osvaldochitumba Palana [Aderito Chosolla, 80’], Manuel Sallo Conha, Antonio Kasule.
REFA: Joseph Odartei Lamptey [Ghana]
CAF KOMBE LA SHIRIKISHO
Raundi ya Mchujo
Ijumaa Mei 6        
Al-Ahli Tripoli – Libya 0 Misr Almaqasa – Egypt 0       
ES Sahel – Tunisia 2 CF Mounana – Gabon 0   
Jumamosi Mei 7         
Young Africans – Tanzania 2 G.D. Sagrada Esperança – Angola 0            
19:00 Mamelodi Sundowns - South Africa v Medeama - Ghana       
20:00 El Merreikh - Sudan v Kawkab Athletic Club Marrakech - Morocco   
20:00 Stade Malien de Bamako – Mali v Fath Union Sport de Rabat - Morocco    
20:00 MO Bejaia – Algeria v ES Tunis - Tunisia         
Jumapili Mei 8         
17:30 TP Mazembe - Congo, DR v Stade Gabesien - Tunisia 
Marudiano
Jumanne Mei 17          
ES Tunis – Tunisia v MO Bejaia - Algeria
Kawkab Athletic Club Marrakech – Morocco v El Merreikh - Sudan   
Stade Gabesien – Tunisia v TP Mazembe - Congo, DR
Fath Union Sport de Rabat – Morocco v Stade Malien de Bamako - Mali    
G.D. Sagrada Esperança - Angola v Young Africans - Tanzania                 
Misr Almaqasa – Egypt v Al-Ahli Tripoli - Libya 
CF Mounana – Gabon v ES Sahel - Tunisia
BAYERN-MUNICH-HISTORIABayern Munich Leo wametwaa Taji lao la 25 la Bundesliga huku wakiwa na Mechi 1 mkononi baada ya kushinda Ugenini Bao 2-1 BUNDESLIGA-MEI18walipocheza na Ingolstadt.

Huu ni Ubingwa wa 4 mfululizo wa Bayern na hii imeweka Historia mpya huku Germany kwa Bayern kuwa Timu ya kwanza kutwaa Ubingwa mara 4 mfululizo.

Bao za Leo za Bayern zilifungwa na Robert Lewandowski na kumfanya aongoze Ufungaji Bora akiwa na Bao 29.

Moja ya Bao za Lewandowski ilikuwa ni Penati na Ingolstadt nao walifunga Bao lao kwa Penati ya Moritz Hartmann.

BUNDESLIGA
Ratiba – Mechi za mwisho za Msimu
Jumamosi Mei 14
Bayer 04 Leverkusen v FC Ingolstadt 04
Bayern Munich v Hannover 96
BV Borussia Dortmund v FC Koln
SV Werder Bremen v Eintracht Frankfurt
VfL Wolfsburg v VfB Stuttgart
FSV Mainz 05 v Hertha Berlin
TSG Hoffenheim v Schalke 04
FC Augsburg v Hamburger SV
Darmstadt v Borussia Monchengladbach

Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
Jumamosi Mei 7
Norwich 0 Man United 1                 
Aston Villa 0 Newcastle 0             
Bournemouth 1 West Brom 1         
Crystal Palace 2 Stoke 1                
Sunderland 3 Chelsea 2                 
West Ham 1 Swansea 4                 
1930 Leicester v Everton            

SUNDERLAND-CHELSEASunderland wamejichomoa toka Timu 3 za mkiaki za BPL, Ligi Kuu England, ambazo hushuka Daraja baada ya kuitwanga Chelsea 3-2 Uwanjani Stadium of Light.

BPL-MEI8
Bao 2 ndani ya Dakika 3 za Kipindi cha Pili ziliipa Sunderland Pointi 3 dhidi ya Chelsea iliyomaliza Mechi hii ikiwa Mtu 10 kufuatia Kepteni wao John Terry kutolewa kwa Kadi Nyekundu Dakika ya 95 baada ya Kadi za njano 2.

Chelsea walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 14 la Diego Costa na Sunderland kusawazisha Dakika ya 41 Mfungaji akiwa Wahbi Khazri lakini Chelsea wakaenda mbele 2-1 Dakika ya 48 kupitia Nemanja Matic.

Bao 2 za Fabio Borini na Jermain Defoe za Dakika za 67 na 70 zikawapa Sunderland ushindi wa 3-2.

Huko Upton Park, West Ham walipata pigo la kufuzu 4 Bora baada ya kunyukwa 4-1 Nyumbani kwao na Swansea City.
Bao za Swansea zilipachikwa na Wayne Routledge, Andre Ayew, Ki Sung-yueng na Bafetimbi Gomis huku West Ham wakifunga kupitia Diafra Sakho.
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba:
**Saa za Bongo
Jumapili Mei 8
1530 Tottenham v Southampton           
[Saa 12 Jioni]
Liverpool v Watford          
Man City v Arsenal           
Jumanne Mei 10
2145 West Ham v Man United              
Jumatano Mei 11
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Norwich v Watford  
Sunderland v Everton                
2200 Liverpool v Chelsea            
Jumapili Mei 15
**Mechi za Mwisho za Ligi, zote kuanza Saa 11 Jioni
Arsenal v Aston Villa         
Chelsea v Leicester          
Everton v Norwich           
Man United v Bournemouth                  
Newcastle v Tottenham              
Southampton v Crystal Palace               
Stoke v West Ham            
Swansea v Man City         
Watford v Sunderland                
West Brom v Liverpool  
KIUNGO wa Simba, Mwinyi Kazimoto, leo anatarajiwa kufunga ndoa na mchumba wake aliyefahamika kwa jina moja la Regina, hivyo hataichezea timu yake dhidi ya Azam FC.


Simba na Azam kesho Jumapili zinacheza mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, ambayo itatoa njia ya bingwa au timu itakayoshika nafasi ya pili.

Kazimoto anatarajiwa kufunga ndoa leo hii katika kanisa moja lililopo Kongowe nje kidogo ya Dar es Salaam, hivyo hataweza kucheza mechi hiyo.

Kwa upande wake Ibrahim Ajib, yeye ataikosa mechi hiyo kutokana na kuwa na kadi tatu za njano alizopata katika mechi zilizopita za timu hiyo.


Kocha wa Simba, Jackson Mayanja, alisema kukosekana kwa wachezaji hao ni pigo kwake lakini amejipanga kuhakikisha anashinda mchezo huo.

BAYERN-MUNICH-HISTORIABayern Munich wapo njiani kuweka historia mpya huko Germany kwa kuwa Klabu ya kwanza kutwaa Ubingwa wa Bundesliga kwa mara ya 4 mfululizo ikiwa wataifunga Borussia Moenchengladbach ndani ya Allianz Arena Jijini Munich.


BUNDESLIGA-TEBO-APR29
Bayern, chini ya Kocha Pep Guardiola, Juzi walifungwa 1-0 na Atletico Madrid kwenye Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI huko Vicente Calderon Jijini Madrid, lakini Jumamosi wanaweza kusahau kipigo hicho na kushangilia.

Huku akilaumiwa kwa kuwapiga Benchi Mastaa wake Thomas Mueller na Franck Ribery kwenye Mechi na Atletico, Guardiola amekataa kusema ikiwa atawapumzisha Mastaa wengine kwenye Mechi hii na Borussia Moenchengladbach kwa sababu ya Marudiano yao na Atletico hapo Jumanne.

Hata hivyo, Mechi hii ya Jumamosi ni nafasi nzuri kwa Beki wao Jerome Boateng kurejea Uwanjani kwa mara ya kwanza tangu Januari alipoumia Nyonga.

Timu iliyo Nafasi ya Pili, Borussia Dortmund, ambayo iko Pointi 7 nyuma ya Bayern huku Mechi zikibaki 3, watakuwa kwao Signal Iduna Park kucheza VfL Wolfsburg.

BUNDESLIGA
Ratiba
**Saa za Bongo
Ijumaa Aprili 29
2130 FC Augsburg v FC Koln
Jumamosi Aprili 30
1630 Bayern Munich v Borussia Monchengladbach
1630 BV Borussia Dortmund v VfL Wolfsburg
1630 Hannover 96 v Schalke 04
1630 FSV Mainz 05 v Hamburger SV
1630 TSG Hoffenheim v FC Ingolstadt 04
1630 Darmstadt v Eintracht Frankfurt
1930 Bayer 04 Leverkusen v Hertha Berlin
Jumatatu Mei 2
2115 SV Werder Bremen v VfB Stuttgart


Timu ya Mgambo ambayo juzi Jumatano ilipoteza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga kwa kufungwa mabao 2-1, imekuwa na rekodi ya aina yake tangu kwa mara ya kwanza ipande kucheza ligi kuu misimu minne iliyopita.

Mgambo ilipanda ligi kuu msimu wa 2012/13 ambapo kwa misimu yote hiyo haikuwahi kushuka daraja, lakini cha kushangaza ni kuwa imefanikiwa kufunga mabao mawili tu ndani ya Uwanja wa Taifa, Dar kwa kipindi hicho chote.

Awali, timu hiyo ilicheza misimu mitatu mfululizo bila ya kuzifumania nyavu za uwanja huo, mpaka walipokuja kuvunja mwiko huo msimu huu walipocheza na Simba Februari 3, 2016 na kukubali kichapo cha mabao 5-1.


Straika wao hatari, Fully Maganga, ndiye aliyefunga dhidi ya Simba na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa timu hiyo kufunga bao kwenye Uwanja wa Taifa, pia juzi Jumatano, Bolly Shaibu Ajally alifanikiwa kufunga bao dhidi ya Yanga likiwa ni la pili kwa timu hiyo ndani ya misimu minne.


JUMAMOSI, ARPILI 30
Everton vs Bournemouth 
Newcastle vs Crystal Palace 
Stoke vs Sunderland 
Watford vs Aston Villa
West Brom vs West Ham
Arsenal vs Norwich 

JUMAPILI, MEI MOSI
Swansea vs Liverpool 
Manchester United vs Leicester 
Southampton vs Manchester City 

JUMATATU, MEI 2

Chelsea vs Tottenham 

MWANASOKA BORA WA ENGLAND, RIYAD MAHREZ ANAYEKIPIGA LEICESTER CITY, RAIA WA ALGERIA.

MWANASOKA BORA KIJANA WA ENGLAND, DELLE ALLI, RAIA WA ENGLAND ANAYEKIPIGA TOTTENHAM

JAMIE VARDY, TUZO YA MWANASOKA ALIYEWEKA REKODI KATIKA UFUNGAJI WA MABAO YAKE.






RYAN GIGGS, NAYE ALIPATA TUZO YA PFA KUTOKANA NA MCHANGO WAKE MWENDELEZO KATIKA SOKA LA ENGLAND.

Na Saleh Ally, aliyekuwa La Coruna
SAFARI ya kwenda Hispania kuliwakilisha Gazeti la Championi ilikuwa ni sehemu ya mafunzo makubwa katika kazi ya uandishi wa habari ambayo inataka mhusika ujifunze kwa wakubwa na wadogo, kila kukicha.

Nilisafiri pamoja na washindi wa “Kwea Pipa Kwenda Hispania na Azam Sports HD”. Ilikuwa ni safari zaidi ya shule ambayo katika mengi niliyojifunza, machache naona yanaanza kwenda kama nilivyoamini.

Kama nilivyoeleza juzi Jumamosi, kwamba mimi na wenzangu kutoka Tanzania pamoja na washindi wengine na waandishi kutoka Hong Kong na Sweden, tulipewa nafasi ya kukaa karibu kabisa wakati wachezaji wa Deportivo La Coruna wakiingia vyumbani. Lakini mwisho tukapewa nafasi kama hiyo kukaa kwenye Mix Zone.
Mix Zone ni sehemu maalum ya waandishi ambayo wanaweza kuwahoji wachezaji kabla au baada ya mechi. Pale mwandishi anachagua mchezaji anayemhitaji na kumuuliza swali analotaka.
Huu ni utaratibu wa kimataifa, kwa wale waliobahatika kuripoti mechi kubwa au michuano mikubwa kama Kombe la Dunia wanajua inavyokuwa.

Wakati wachezaji wanaingia vyumbani, kulikuwa na ulinzi mkali na watu wengi waliwekwa hatua takribani 50 upande wa pili wa barabara tofauti na sisi ambao tungeweza hata kupeana nao “tano”.

Wakati wachezaji wakishuka, hata kabla ya kufika pale tulipo, ilikuwa ni rahisi kujua aliyeshuka ni nyota kweli, maana watu walipiga kelele za juu zaidi na baada ya muda ungemuona mchezaji huyo anakuja upande wetu.
Walioongoza kushangiliwa walikuwa ni Iniesta, Lionel Messi halafu Neymar ambaye alibaki ndani ya basi peke yake kwa takriban dakika 5, ndiyo akashuka taratibu kabisa.

Luis Alberto Suarez Diaz, alishangiliwa kwa kiwango cha kati. Lakini ushukaji wake kidogo ulinishangaza, kwani alishuka haraka sana na kukimbia kama mtu ambaye alikuwa akihofia kukamatwa.

Uso wake alionekana kama mtu asiyetaka kuonekana au kuzungumza na mtu. Hakutabasamu kama wachezaji wengine, hakuonyesha urafiki na yeyote na aliwapita wachezaji wenzake waliowahi kuteremka kwenye basi na kuwahi kuingia vyumbani.

SUAREZ AKISAINI JEZI ALIYOPEWA NA SALEH ALLY

Kwa kuwa nilikuwa na baadhi ya waandishi wa Hispania, nilimuuliza mmoja kwamba hiyo ni tabia ya kawaida ya Suarez? Akanijibu:

“Kawaida hapa Hispania, wachezaji hawaruhusiwi kuzungumza kabla ya mechi, hofu ni kwamba unaweza kuwapotezea ‘focus’ (uwezo wa kulenga jambo wanalotaka kulifanya kwa ufanisi).

“Lakini Suarez yuko hivyo, ana hasira na anataka kufunga kila mechi ikiwezekana zaidi ya mabao mawili.

“Ukiwa unataka kumhoji, omba afunge. Kama itakuwa Barcelona imefungwa au hajafunga, usimsogelee kabisa, huwa hazungumzi na mara nyingi anakuwa wa kwanza kupanda kwenye basi.”

Hakuendelea kunipa maelezo kwa kuwa tulitakiwa kuondoka eneo hilo na kwenda kupiga picha na wachezaji wa Deportivo La Coruna waliokuwa benchi. Kwa upande wa wachezaji wa Barcelona, tulielezwa kwamba lilikuwa jambo gumu. Hivyo tukafanya hivyo.



Niliangalia mechi nikiwa makini na mambo mengi, lakini maelezo ya Suarez yalinifanya niwe makini sana kwake kwa muda wote wa mechi nikitaka kujua atafanya nini. Alikuwa ndiye mwiba kwa walinzi wa Deportivo La Coruna, akafunga mabao manne, Barcelona ikishinda kwa mabao 8-0.

Wakati wachezaji wanatoka tukiwa katika Mix Zone, nilisubiri atokee Suarez kuthibitisha yale maelezo ya mwandishi kutoka gazeti namba moja la michezo Hispania la Marca.


Alipotoka tu, nilikuwa mtu wa kwanza kumuita. Alitoa ushirikiano kwa kusaini jezi yangu na kujibu swali nililomuuliza. Hakika alionekana ni mwenye furaha, alipiga picha na watoto wawili, halafu akasogea na kupiga picha na mtu mmoja ambaye alimuomba, nikaamini hilo.

Lakini njaa ya Suarez ikaanza kubadili mawazo yangu, kwamba hata Barcelona wenyewe hawaoni kwa kuwa staa mkubwa au tegemeo zaidi kwao ni Suarez, tena kwa sasa anazidi hata umuhimu wa Neymar na Messi.

Utaona baada ya mechi hiyo, iliyofuatia niliishuhudia kwenye runinga, Barcelona wakiwa nyumbani Camp Nou, wakaigaragaza Sporting Gijon kwa mabao 6-0, Suarez akapiga mengine manne, safari hii akiwa na mawili ya penalti.

Suarez ana njaa kweli na ukiangalia, uwanjani utaona ana tofauti kubwa. Kikubwa kinachomsaidia hachezi kama supastaa. Anakimbiza mpira, anakaba, anabugudhi na anapambana muda wote, jambo ambalo ni nadra kumuona Messi, Neymar au hata Cristiano Ronaldo akifanya hivyo.


Ndani ya mechi mbili, kafunga mabao 8. Sasa ndiye anaongoza kwa ufungaji. Kabla ya mechi hizo mbili alikuwa anazidiwa na Ronaldo mabao matano. Sasa anamzidi mshambuliaji huyo nyota wa Real Madrid mabao matatu. Yeye kapiga 34 na Mreno huyo 31.

Awali ilionekana ni vita ya Messi na Ronaldo, sasa Suarez kaingia katikati na huenda akawa ndiye staa namba moja kuliko wote na huenda baada ya msimu huu akawa ndiye gumzo kuliko wote kama alivyoondoka England akiwa tegemeo na gumzo kuliko wote.

Awali ukizungumzia mabao na pasi, ungemtaja Messi. Lakini Suarez anadhihirisha anajua mno mpira na ndiye baba mpya mwenye nyumba wa Barcelona, yaani tegemeo, kwani baada ya kucheza dakika 2880 za La Liga, kafunga mabao 34 akiwa ametoa pasi 15 zilizozaa mabao. Kama hiyo haitoishi, katika dakika hizo amepiga mashuti 115 na 62 yamelenga lango.

Utaona takwimu zake ziko juu hata kuliko Ronaldo aliyecheza dakika 3059, akafunga mabao 31 na kutoa pasi 11 tu za mabao.

Messi naye amecheza dakika 2458, amefunga mabao 25 na pasi 13 za mabao. Neymar amecheza dakika 2787 na kufunga mabao 23 na pasi 10 zilizozaa mabao.

 Maana yake kama utazungumzia mabao na pasi za mabao au asisti, Suarez hadi sasa ni bora zaidi ya Ronaldo, Messi na Neymar.

Ndiyo anakwenda msimu wa pili wa La Liga, lakini anaonyesha si mtu wa kawaida. Suarez aliyetoka England kama mkosaji, Barcelona wakaonekana kama “wamebugi”, sasa ndiye shujaa mpya wa Blaugrana.


Huyu jamaa, anajua sana. Mbishi, si mwepesi kukubali na anachotaka ni kushinda zaidi ya mara moja, kufunga mabao zaidi ya yanayotegemewa na hii haina ubishi, atakuwa hashikiki na ndiye shujaa mpya wa Barcelona, hasa kama hataharibu na yale mambo yake.

TAKWIMU LA LIGA:
WATANO WANAOONGOZA LA LIGA KWA MABAO:

Luis Suárez
Barcelona
Amecheza dakika 2880  
Mabao 34
Asisti 15 

Cristiano Ronaldo
Real Madrid
Amecheza dakika 3059  
Mabao 31
Asisti 11 

Lionel Messi
Barcelona
Amecheza dakika 2458
Mabao 25
Asisti 13 

Neymar
Barcelona
Amecheza dakika 2787  
Mabao 23
Asisti 10 

Karim Benzema
Real Madrid
Amecheza dakika 1838 
Mabao 23
Asisti 6


SOURCE: CHAMPIONI