SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

MICHEZO


Manchester City (4-2-3-1): Hart 7, Maffeo 6.5, Stones 7 (Adarabioyo 60, 6), Kolarov 6.5, Clichy 6, Toure 7, Fernando 6, Delph 6.5, Jesus Navas 6, Iheanacho 7.5 (Fernandinho 76), Nolito 6 (Tasende 60, 6)
Subs: Gunn, Sterling, Aguero, Silva
Goals: Delph 56 
Steaua Bucharest (4-5-1): Cojocaru 6.5; Aganovic 6 (Stanciu 53 6.5), Tamas 6.5, Mitrea 6.5, Momcilovic 6; Enache 6, Sulley 6 (Achim 62 6), Bourceano 7, O Popescu 6 (Popa 53 6), Hamroun 6; Tudorie 6
Subs not used: Nita, Simion, Valceanu, D Popescu 
Man of the match: Iheanacho 
Referee: Pawel Gil 6 (Poland)
*Ratings by Joe Bernstein at the Etihad Stadium 








SALVATORY EDWARD
Kiungo wa zamani wa timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Ngawina Ngawina, pamoja na kiungo wa zamani wa Yanga, Salvatory Edward wameanzisha kituo cha kuibua vipaji vya wanasoka chipukizi chini ya umri wa miaka 17 na kuviendeleza.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ngawina alisema kituo chao kinaitwa Kambiasso Sports na kwamba kwa kuanzia Jumamosi wiki hii watafanya kliniki maalum ya kusaka vipaji hivyo kwenye Uwanja wa Tandika Mabatini, Dar es Salaam, dhamira yao kubwa ikiwa ni kuhakikisha wachezaji wenye vipaji wanaendelezwa na kutafutiwa timu.

“Kila mzazi mwenye mtoto ambaye anaamini ana kipaji cha soka na anahitaji aendelezwe, amlete mwanae Tandika Mabatini Jumamosi Agosti 27, ajitahidi saa mbili asubuhi awe ameshafika, kwani ndiyo muda tutakaoanza.

“Kliniki yetu itaendeshwa na makocha mahiri, ambao wana leseni za ukocha kutoka Caf (Shirikisho la Soka Afrika), ili kufanya hili jambo kiuweledi zaidi na kupata vijana wenye sifa,” alisema Ngawina.

Alisema dhamira yao ni kupata vijana wengi wenye vipaji kadri iwezekanavyo na kwamba suala la idadi itategemea na watakavyoona siku hiyo, lakini dhamira yao ni kuwa na vijana wasiopungua 30, lakini si lazima wote wapatikane Dar es Salaam, wataenda hadi mikoani.

Aliwataja watakaoendesha mshujo huo licha ya yeye na Salvatory, pia atakuwepo kocha Kennedy Mwaisabula, ambaye amepata kufundisha timu mbalimbali nchini ikiwemo Yanga.

Mwingine ni kipa wa zamani wa timu mbalimbali ikiwemo Simba ya Dar es Salaam na Ferroviario De Maputo ya Msumbiji, Muharami Mohammed ‘Shilton’, ambaye kwa sasa ni kocha wa makipa wa timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ . Pia atakuwepo kocha mwingine wa makipa Terry Muhorel.

“Soka si kama paa la nyumba kwamba siku zote linakuwa juu tu. Soka inaanzia chini na ndiko tunakotaka twende,” alisema Ngawina.

Kwa upande wake Salvatory alisema dhamira yao ni kuwa na kituo ambacho kitakuwa hazina ya nchi kwa wachezaji wa siku za usoni, lakini pia kiwe kitovu cha timu mbalimbali kuchukua wachezaji.

“Tunaamini vijana wetu wakishaiva tutawauza timu mbalimbali za ndani ya Tanzania na nje, kwani kituo kina uhusiano mzuri na watu mbalimbali waliopo hapa nchini na hata nje ya nchi,” alisema Salvatory.

 “Tunaosimamia jambo hili tumecheza mpira kwa kiasi cha kutosha, tumesomea ukocha, tunajua nini cha kufanya kuendeleza vijana wetu,” alisema.

Aliwaomba wachezaji chipukizi wa umri huo wanaoamini wana uwezo wajitokeze siku hiyo ili kuwania nafasi ya kuwepo katika kituo hicho ambacho kitakuwa Temeke, Dar es Salaam.

Baada ya kikosi cha Mwadui FC kuchapwa kwa bao 1-0 katika mechi yao ya Ligi Kuu Bara, kocha wake, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameamka na kusema, anakubali kufungwa lakini akasisitiza, walicheza mechi kwenye uwanja mbovu.

Toto African ndiyo walioichapa Mwadui FC kwa bao 1-0, katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Dar es Salaam. Shujaa wa Toto akiwa ni Waziri Junior aliyepachika bao hilo katika kipindi cha kwanza.

“Nakubali kabisa kuwa mchezo nimepoteza kwa kuwa bao lilikuwa hakuna lawama hata  kidogo. Tumepambana mwisho ukashindikana.

“Lakini uwanja tuliochezea, unaweza ni wa kuchezea ng’ombe na si binadamu. Hauna viwango na kweli umeharibika sana.

“Awali tulikuwa tucheze Jumamosi, eti mechi ikaahirishwa kwa kuwa kuna Fiesta na ajabu ligi ilishapangwa, kwa kuwa kuna shughuli ambayo si ya soka, mechi inaahirishwa,” alisema Julio.

Katika mechi hiyo, Mwadui FC walishindwa kung’ara katika kipindi cha kwanza, lakini wakacharuka katika kipindi cha pili lakini hakukuwa na mafanikio.


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeweka bayana kuwa, lipo kwenye mpango wa kuwakabidhi kombe jipya la Ngao ya Jamii timu ya Azam kutokana na kukabidhiwa kombe ambalo halikuwa lenyewe.

Azam waliichapa Yanga kwa penalti 4-1 katika mchezo wa Ngao ya Jamii baada ya kumaliza dakika tisini kwa sare ya mabao 2-2, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar. 




  Msemaji wa TFF, Alfred Lucas ameliambia Championi Jumatano kuwa, waliwapa Azam ngao ambayo siyo yenyewe kutokana na kuchelewa kukamilika kwa utengenezwaji wa ngao halali ambalo walitakiwa kupewa.

“Lile kombe ambalo tuliwapa Azam siku ile walipocheza na Yanga kwenye Ngao ya Jamii halikuwa lenyewe, bali tulilitoa kwa ajili ya kuziba nafasi ya kombe halisi ambalo lilichelewa kuja kutokana na kutokamilika mpaka inafika siku ile, hivyo tukaona siyo vizuri bingwa akiondoka mikono mitupu.

“Tumepanga kuwabadilishia na kuwapa kombe lao halisi ambalo walistahili kupewa ambalo hili litakuwa na thamani halisi na mwonekano tofauti kabisa na lile ambalo tulilitoa awali,” alisema Alfred.

SOURCE: CHAMPIONI
Kiungo wa Manchester United, Mjerumani Bastian Schweinsteiger, amesema baada ya kuondoka ndani ya kikosi hicho, hafikirii kujiunga na timu nyingine ya barani Ulaya, na badala yake ataenda kucheza soka katika Ligi ya Marekani au Asia.

Schweinsteiger ambaye amekuwa hafanyi mazoezi na kikosi cha kwanza cha United kutokana na kutokuwepo kwenye mipango ya kocha wa timu hiyo, Jose Mourinho, bado ameonyesha nia ya kuendelea kubaki klabuni hapo.

Kupitia akaunti yake ya Mtandao wa Kijamii wa Twitter, Schweinsteiger aliandika: “Manchester United itakuwa klabu yangu ya mwisho hapa Ulaya. Naziheshimu klabu zingine, lakini Manchester United ndiyo timu pekee iliyonifanya nikaihama Bayern Munich. Nipo tayari kubaki kama timu hii itaendelea kunihitaji.



 


“Hiki ndicho ninachoweza kukisema kuhusiana na hatma yangu ya sasa. Napenda kuwashukuru mashabiki kutokana na ushirikiano waliouonyesha kwangu.”

Mjerumani huyo aliyekuwa kwenye kikosi cha Ujerumani kilichotwa ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2014, mshahara wake ndani ya United ni pauni 160,000 kwa mwaka na mkataba wake umebakia miaka miwili kumalizika.


Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ametangaza kikosi cha wachezaji kikiwa na mabadiliko kadhaa ambacho atakiandaa maalumu kwa mchezo dhidi ya Nigeria.

Kikosi hicho kina wachezaji 20 ambao atasafiri nao kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo huo wa Septemba 3, 2016 lakini wachezaji wanatakiwa kuripoti kambini Agosti 28, mwaka huu na safari ya kwenda nchini Nigeria itakuwa Septemba mosi.

   


KIKOSI HICHO HIKI HAPA:
Deogratius Munish ‘Dida’
Aishi Manula
Mwinyi Haji
Andrew Vincent ‘Dante’
Juma Mahadhi
Kelvini Yondani
David Mwantika
Himid Mao
John Bocco
Farid Mussa
Jamal Mnyate
Ibrahim Ajib
Shiza Kichuya
Mzamiru Yassin
Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’
Jonas Mkude
Mbwana Samatta
 Ibrahim Rajabu
Shomari Kapombe
Simon Msuva
HANS POPPE

Ikiwa ni siku chache baada ya Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kumtaka beki Hassan Kessy kuondoa hofu kwa kuwa siku itafika atacheza, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema huenda beki huyo akaendelea kubaki nje ya uwanja kwa msimu huu na mwingine.

Manji alisema hayo juzi huku akisisitiza, Kessy hawezi kutocheza milele.

Lakini Hans Poppe amesema kinachomponza Kessy ni ujeuri wa viongozi wa Yanga ambao wanajua wamekosea, lakini wanataka kuonyesha umwamba.

Akifanya mahojiano na SALEHJEMBE jijini Dar es Salaam, Hans Poppe amesema Yanga wanajua wamefanya makosa, lakini wanataka kuonyesha umwamba kama walivyozoea.

“Waliwahi kutufanyia hivi katika suala la Yondani, safari hii wamerudia na kumsainisha Kessy wakati akiwa bado na mkataba na Simba.


“Kama hiyo haitoshi, mkataba wameufikisha TFF, wameusajili na wakatuma Caf. Sasa sisi tuna kila kitu na ushahidi mwingine wao wenyewe wameupeleka TFF na Caf.
“Kilichotakiwa ni kuandika barua, nilikutana na Chanji (kiongozi Yanga). Nikamweleza andikeni barua mimi nitalisimamia hilo. Lakini hakufanya hivyo, wanataka kuonyesha ujeuri.

“Kama itaendelea hivi, ninaamini Kessy hatacheza. Na hapa wa kulaumiwa ni wao maana Simba tupo hapa,” alisema Hans Poppe na alipoulizwa kama wakiandika barua basi mara moja watamruhusu Kessy, akajibu.


“Wakiandika barua, basi sisi tuna jibu au majibu ya kuwapa. Sasa yatapatikana kutokana na barua yao.”





MAMA MZAZI WA POGBA AMENUNUA RUNDO LA JEZI ZA MWANAYE MARA TU BAADA YA KUANZA KUINGIA MTAANI IKIWA NI SAA CHACHE BAADA YA KUJIUNGA NA MAN UNITED AKITOKEA JUVENTUS.

IMEELEZWA MAMA HUYO ANAJIANDAA KUTOA ZAWADI KWA WATU MBALIMBALI AMBAO NI WATU WAKE WA KARIBU. POGBA RAIA WA UFARANSA AMEJIUNGA NA MAN UNITED KWA KITITA CHA PAUNI MILIONI 100.