SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

Latest Post


Manchester City (4-2-3-1): Hart 7, Maffeo 6.5, Stones 7 (Adarabioyo 60, 6), Kolarov 6.5, Clichy 6, Toure 7, Fernando 6, Delph 6.5, Jesus Navas 6, Iheanacho 7.5 (Fernandinho 76), Nolito 6 (Tasende 60, 6)
Subs: Gunn, Sterling, Aguero, Silva
Goals: Delph 56 
Steaua Bucharest (4-5-1): Cojocaru 6.5; Aganovic 6 (Stanciu 53 6.5), Tamas 6.5, Mitrea 6.5, Momcilovic 6; Enache 6, Sulley 6 (Achim 62 6), Bourceano 7, O Popescu 6 (Popa 53 6), Hamroun 6; Tudorie 6
Subs not used: Nita, Simion, Valceanu, D Popescu 
Man of the match: Iheanacho 
Referee: Pawel Gil 6 (Poland)
*Ratings by Joe Bernstein at the Etihad Stadium 






WANAUME wawili wanaoishi kama mume na mke (mashoga) nchini Afrika Kusini wanasemekana kuwa watu wa kwanza katika ukanda huo na huenda duniani kwa kuwa wazazi wa mapacha watatu, wawili wakiwa wanafanana, kwa kupitia mtu mwingine aliyebeba mimba.

Wazazi hao ambao walikuwa majirani na mwanamichezo za zamani mlemavu, Oscar Pistorius, walikutana na mtu waliyempatia mbegu zao wakati wa mashitaka ya mauaji yaliyokuwa yanamkabili.
Christo na Theo Menelaou wamewachukua watoto wao nyumbani kwao mjini Pretoria baada ya kukaa hospitali kwa wiki tatu za matatizo.  Kutokana na kuzaliwa kabla ya wakati wao, Julai 2, mapacha hao walijikuta maisha yao yakining’inia kati ya uhai na kifo.

couple (1)Joshua alikuwa mtoto wa kwanza kuzaliwa kwa njia ya upasuaji na ndiye alikuwa mzito kuliko wote akiwa na uzito wa kilo 1.8; Zoe alifuatia akiwa na kilo 1.3 na Kate aliyekuwa na kilo 1.3 pia.

Watoto hao waliwekwa kwenye mashine za kuwasaidia kupumua hadi walipokuwa na nguvu za kutosha na kuweza kuondoka katika hospitali ya Sunninghill ya Johannesburg.

Waliondoka siku tofauti kwenda nyumbani, ambapo Joshua alikuwa wa kwanza kuruhusiwa siku ya Julai 22,  akafuata Zoe aliyeruhusiwa siku kumi baadaye na Kate ambaye aliruhusiwa Agosti 4.
Christo Menelaou aliliambia shirika la utangazaji la Sky News: “Ukiwa shoga, siku zote unafikiri kwamba haiwezekani ukawa mzazi hata kama una upendo kiasi gani.

“Ni vigumu kupewa mtoto wa kuasili na kila mara tuliambiwa kwamba ni wazazi wa kawaida tu ndiyo huruhusiwa.  Pia hatukuweza kufikiri kwamba tungempata mtu ambaye angekubali kubeba mbegu za mashoga.

Hata hivyo, mama mmoja mwenye watoto watatu, waliyekutana naye wakati wa mashitaka ya Pistorious, alikubali kutubebea mbegu zetu.”

Sheria za Afrika Kusini kuhusu upandikizaji wa mbegu kwa watu wengine, iliwataka wanaume wote wawili hao, mtu mwenye kubeba mbegu zao na mumewe wasaini mkataba mbele ya jaji kusisitiza kwamba walikubaliana kwa hiari katika jambo hilo na kwamba pasingekuwepo na kupeana fedha au kubeba gharama zozote.

Wawili hao walikwenda kwenye benki ya mayai na kuchagua mayai  ambapo yai moja lilirutubishika  na mbegu ya Christo na kuwekwa katika tumbo la mbeba mimba na baadaye aliwekewa yai lililokuwa na mbegu ya Theo.

Baada ya wiki kumi za mimba hiyo, uchunguzi ulionyesha kwamba moja ya mayai hayo yaliyorutubishika lilikuwa limejitenga na mbeba mimba alikuwa ana mapacha watatu, wawili wakiwa ni wenye kufanana.

Wakati ambapo madaktari wengi waliwashauri wanaume hao kwamba mbeba mimba huyo akatishe uhai wa mapacha wawili ili kutoa fursa ya mtoto wa tatu kuendelea bila matatizo, hatimaye walimpata mtaalam wa masuala ya watoto ambaye alisema angewasaidia jinsi ya kuhakikisha watoto hao wanazaliwa salama.

Dk Heidra Dahms, ambaye ni mtaalam wa masuala ya watoto katika Hospitali ya Sunninghill na aliyesimamia kuzaliwa kwa watoto hao, aliliambia shirika la Sky News : “Ni jambo adimu sana.  Sijawahi kusikia kitu kama hicho hata siku moja.”

Watoto walikuwa ni wadogo mno, mapafu yao yalihitaji msaada wa ziada ili kupumua na Theo alilazimikakulala kando ya kitanda hadi walipopata nguvu.

Hata hivyo, wazazi hao wanakabiliwa na changamoto ya kumfanyia upasuaji Zoe kutokana na kasorokwenye moyo, upasuaji ambao unahitajika kufanyika katika kipindi cha miezi sita.
Pamoja na yote hayo, wawili hao  wanasherehekea kuitwa ‘baba’, jambo ambalo hawakutegemea kamwe lingewezekana.

Hivi sasa wanaendelea kuwatunza watoto wao hao watatu nyumbani kwao kwa msaada wa mayaya wawili usiku na mchana ambapo kila mtoto amefungwa kidude kinachotoa sauti iwapo watashindwa kupumua.

Theo alisema: “Tunalazimika kuwasugua taratibu kwenye migongo yao au kutekenya vidole vyao ili kuwakumbusha kupumua.

“Tunajisikie tumebarikiwa sana,” alisema kwa furaha.
CHAMA cha Tanzania Labour(TLP) kimemuandikia barua Rais wa Mapinduzi wa Zanzibar, Dk Mohamed Ali Shein na kumtaka kuanzia sasa wamtenge Katibu Mkuu wa CUF , Maalim Seif Sharif Hamad (pichani), kwa kutomualika kwenye shughuli zozote za kitaifa mpaka atakapojirekebisha na kuitambua rasmi serikali iliyopo madarakani.

Aidha, kwa kuwa CUF inadai kwamba haiitambui serikali hiyo basi ruzuku kwa chama hicho isitishwe kuanzia sasa hadi hapo chama hicho kitakapoitambua rasmi serikali hiyo na kuacha kuhamasisha wananchi wasilipe kodi.

Katika barua ya chama hicho iliyosainiwa na Mwenyekiti wake, Augustine Mrema ilisema chama hicho kimesikitishwa na wanalaani kitendo kilichofanywa Hamad ambaye pia alikuwa Makamu wa kwanza wa Rais kwenye serikali ya Umoja wa kitaifa wa Zanzibar (SUK) wakati wa maziko ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa serikali ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar, marehemu Mzee Aboud Jumbe cha kukataa kumpa Rais Shein mkono wa kusalimiana.

Alisema kuleta tofauti za kisiasa msibani kwa makusudi, Maalim Seif ameendelea kuwagawa Wazanzibari kisiasa na kushindwa kumuenzi marehemu Aboud Jumbe, ambaye pamoja na kuiongoza Zanzibar kwa amani na utulivu pia ndiye aliyemlea Maalim Seif kisiasa.

Alisema tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa marudio uliosusiwa na CUF, Maalim Seif amekuwa akileta chokochoko na uchochezi dhidi ya serikali ya Zanzibar akidai kwamba haitambui na kuwataka wananchi wa Zanzibar kugoma na kuwataka wasilipe kodi kwa serikali
Kwanza ninawapa pole familia za Polisi wote waliouwawa waliokuwa kwenye majukumu yao ya ulinzi wa raia na mali zao.

Ni huzuni kubwa Polisi kuuwawa na silaha kwenda kwenye mikono ya wahalifu, tukio kama hili ni muhimu likatukumbusha kwamba Taifa linaweza kujengwa vyema kama kila mmoja atawajibika katika haki na sheria , kumbe Polisi wanaweza kuuwawa na Watu wasio na huruma na wasiotii sheria , kama ambavyo Polisi wasio na huruma na utii kwa Katiba wanavyoweza kujiandaa kuvunja ukuta unaotaka uwajibikaji wa matumizi sahihi ya Katiba na sheria.

Ni ishara mbaya sana kuona walinzi wetu wanauwawa, lakini ni ishara mbaya zaidi kuona walinzi wetu wakiwa kwenye mazoezi hadharani ya kujipanga kudhibiti na pengine hata kuua Wananchi wanaodai haki yao Kikatiba ya mikutano ya vyama vya Siasa.

Uimara wa Jeshi letu utajengwa na uhusiano mzuri kati yake na raia na sio silaha za kisasa na mazoezi ya vitisho hadharani.

Poleni sana Watanzania kwa tukio hili baya, ni matumaini yangu kuwa watu hawa watatiwa nguvuni haraka iwezekanavyo.
Kwa hili linalotokea kwa Diamond kwa sasa ni kama kero kwa baadhi ya watu lakini ni sherehe kwa upande wa mashabiki wake kutokana na kila siku anaibuka na stori mpya na kubwa ambazo zinateka vichwa vya habari.

Baada ya hapo jana stori ya kumpatia zawadi ya gari Raymond kukiki, leo yameibuka mapya na makubwa zaidi baada ya hitmaker huyo wa Kidogo kuonekana akiwa na staa wa Nigeria, Wizkid huku mashabiki wakijiuliza nini kinaendelea?

Vipande viwili vya video alivyopost Diamond kwenye mtandao wake wa Instagram akiwa na staa huyo wa Nigeria vimewashtua mashabiki kutokana na hitmaker huyo wa ‘Shaba’ kwa sasa siyo msanii wa kitoto kwa kuwa muziki wake tayari tayari umepenya nchini Marekani na tayari ameshafanikiwa kufanya collabo na mastaa wa nchi hiyo akiwemo Swizz Beat, Drake na Chris Brown.


Haikuwa ngumu kwa hitmaker wa ‘Kidogo’ kukutana na staa huyo kutokana tayari wameshakutana mara kadhaa ikiwa ni pamoja na kufanya show kwenye jukwaa moja ikiwemo ile ya ‘One Africa’ iliyofanyika nchini Marekani mwezi uliopita pamoja na ile iliyofanyika nchini mwaka jana kwenye viwanja vya Leaders Club.

Hata hivyo inadaiwa kuwa vipande hivyo vya video vinavyowaonyesha wasanii hao walikutana Afrika Kusini na siyo Bongo kama watu wanavyofikiria kwakuwa huenda Wizkid aliondoka Dar August 22.
Mr Blue amekiri kuwa skendo yake kuwa amekuwa akiwasiliana na ex wake, Naj ambaye kwa sasa ana uhusiano na Barakah Da Prince ilitaka kuivunja ndoa yake.

Akiongea na Clouds FM, rapper huyo wa ‘Mboga Saba’ amedai kuwa mke wake, Wahyda sasa amekuwa na wivu wa kufa mtu tangu kuzuke skendo hiyo.

“Sasa hivi naona kama wivu umezidi baada ya hii skendo ya hawa jamaa kuitengenezea kiki kwasababu wanataka kutoa nyimbo yao, skendo kwamba mimi nilimpigia yule mwanamke mwingine nani anaitwa, Najma yule. Wametengeneza kweli kabisa, mimi nimezipata za kunyapianyapia kwamba wametengeneza ili kukikisha nyimbo zao,” amesema Blue.
“Lakini wamenikosea sana kwasababu wanataka kugombanisha ndoa yangu, mimi nina mke ujue, siwezi kumpigia mtu ambaye nimemwacha, ni kosa kubwa sana, halafu mke wangu yule ni mwanamke ambaye walikuwa watatu kupigania nani awe na mimi, yaani bora hata ningempigia mtu mwingine,” amesisitiza.

“Ilifika karibu kama siku mbili tuna ugomvi mimi na mke wangu, ni kitu kikubwa sana, nimekasirika sana, nimechukia sana na nawaambia mashabiki wangu, alichokifanya Barakah na watu wake, kama sio yeye simlaumu, kama watu wake nilikuwa naomba waoneshe proof kwenye mitandao waoneshe namba yangu niliyompigia, waioneshe kwamba ni hiyo kweli sio unaongeaongea tu.”