Mahakama Kuu kupitia Mheshimiwa Jaji IGNAS KITUTSI asubuhi ya jana
imetupilia mbali maombi madogo ya kesi ya kuomba kupunguziwa gharama za
dhamana ya kesi iliyofunguliwa na mwanasiasa Jonas Nkya dhidi ya
msanii/mbunge Joseph Haule (Profesa Jay).
Mahakama imetupilia mbali kesi hiyo na kukubaliana na hoja za
mapingamizi ya kisheria yaliyowekwa na jopo la mawakili wa msanii huyo –
Tundu Lissu na John Mallya.
Mahakama pia imemuamuru mlalamikaji Jonas Nkya ambaye walikuwa
wakigombea pamoja nafasi ya ubunge wa jimbo la Mikumi alipe gharama zote
za kesi na usumbufu.
Hakuna maoni :