Lakini Jumamosi zipo Mechi 7 ikiwemo ile ya Mabingwa Watetezi Chelsea kucheza na
Kibaya zaidi ni kufungwa kwa Chelsea huko Ureno Bao 2-1 Juzi Jumanne na FC Porto kwenye Mechi ya Kundi lao la UEFA CHAMPIONZ LIGI na hii imezidisha presha kwa Mabingwa hao.
Hiyo hiyo Jumamosi, Man City wako kwao Etihad kucheza na Newcastle huku wao pia wakikodolewa mimacho baada ya kuanza vyema Ligi kwa kushinda Mechi 5 mfululizo wakipaa kileleni na kisha kuporomoka kwa kufungwa Mechi mbili zilizopita.
Jumapili Mechi ya kwanza ni huko Goodison Park Jijini Liverpool, ikiwa ni Dabi ya Merseyside, inayozikutanisha Wenyeji Everton na Mahasimu wao wa Jadi Liverpool.
Baada ya Dabi hii zipo Mechi mbili zinazoanza muda sawa kati ya Swansea na Tottenham lakini jicho litakuwa huko Emirates kwenye mtanange mkali kati ya Arsenal na Manchester United.
Baada ya Mechi hizi za Wikiendi hii, Ligi Kuu England itapumzika kupisha Mechi za Kimataifa na kurudi tena hapo Oktoba 17.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumamosi Oktoba 3
1445 Crystal Palace v West Brom
1700 Aston Villa v Stoke
1700 Bournemouth v Watford
1700 Man City v Newcastle
1700 Norwich v Leicester
1700 Sunderland v West Ham
1930 Chelsea v Southampton
Jumapili Oktoba 4
1530 Everton v Liverpool
1800 Arsenal v Man United
1800 Swansea v Tottenham

Hakuna maoni :