SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / Bendera ya Palestina yapandishwa kwenye Umoja wa Mataifa



Makao makuu ya Umoja wa Mataifa, mjini New York.
Makao makuu ya Umoja wa Mataifa, mjini New York.
Jumatano hii, Septemba 30, bendera ya Palestina itapandishwa kawa mara ya kwanza mbele ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. Palestina iliteuliwa mwaka 2012 kuwa mwangalizi katika Umoja wa Mataifa, lakini ilichukua hadi katikati mwa mwezi Septemba ili kuruhusu bendera yake kuelea mbele ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa.



Huu ni ushindi wa kidiplomasia kwa mamlaka ya Palestina, lakini jambo hili linashutumiwa na wawakilishi wa Israel katika Umoja wa Mataifa. Katika Majimbo Yanayokaliwa, wakati baadhi ya wanakaribisha hatua hii mpya kuelekea kutambuliwa kimataifa kwa taifa la Palestina, watu wengi wanajua kwambahali hii haitoleta mabadiliko katika maisha yao ya kila siku.

Vita nchini Syria, harakati za makundi ya kigaidi au mgogoro wa wahamiaji vinawatia wasiwasi viongozi na marais wanaohudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York kama hali inayoendelea majimbo ya Gaza na Cisjordania, amearifu mwandishi wetu nchini Marekani, Anne Corpet, ambaye amekumbusha kwamba sababu ya Palestina, kuwepo katika mkutano huo, kumepelekea iwekwe katika agenda ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Mwaka huu.

Kwa karibu miaka 70, suala la Palestina lilipelekea kuchukuliwa maazimio mengi katika Umoja wa Mataifa, ambapo ilipewa kipaumbele katika mijadala mbalimbali. Baadhi ya maazimio hayo licha ya kuwa ni machache yalitekelezwa, na miradi mingi ilijikuta ikikabiliwa na upinzani mkubwa wa kura ya turufu ya Marekani. 

Katika hotuba inayosubiriwa sana kwenye jukwa la Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jumatano wiki hii, Rais wa Mamlaka ya Palestina atachukua nafasi hiyo kwa kuiomba jumuiya ya kimataifa kuchangia juu ya hatma ya watu wake

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply