Itifaki
ya makubaliano kwa lengo la kurudisha taasisi za mpitoimegonga vishwa
kwenye magazeti mbalimbali nchini Burkina Faso Jumatatu hii Septemba
21, 2015, Ouagadougou.
Nchini Burkina Faso, vikosi vya jeshi tiifu kwa serikali ya
mpito iliyopinduliwa na wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa Rais, wako
njiani Jumatau wiki hii kuelekea katika mji mkuu wa nchi hiyo,
Ouagadougou.
Wanajeshi hao wanatokea pande tatu wakielekea kukabiliana na
wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa Rais waliofanya mapinduzi ya serikali.
makundi ya wanajesh yanatokea magharibi mwa nchi (Dedougou na Bobo
Dioulasso), Mashariki (Kaya na Fada N'Gourma) na kaskazini (Ouahigouya)
na yanaelekeakatika mji mkuu wa Ouagadougou.Katika taarifa yao, wakuu wa vikosi vya jeshi la taifawamewaomba wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa Rais (RSP) " kuweka chini silaha zao na kurejea katika kambi ya Sangoulé Lamizana. Wao na familia zao watalindiwa usalama ".
Hali ya wasiwasi bado imetanda katika mji mkuu wa Ouagadougou.
Viongozi wa mapinduzi hayo ni washirika wa karibu wa Rais Blaise Compaoré aliyeondolewa mamlakani kufuatia maandamano ya raia mwaka uliyopita.
Walinzi hao wa Rais walitekeleza mapinduzi hayo baada ya kuvamia mkutano wa baraza la mawaziri Alhamisi iliyopita uliokuwa ukiongozwa na Rais Kafando na Waziri Mkuu Isaac Zida Alhamisi.
Rais Kafando aliachiliwa huru baadaye lakini hatima ya Isaac Zida bado haijulikani.
Walinzi hao wa Rais walimtangaza Jenerali Gilbert Diendéré kuwa kiongozi wao.
Wakati huo huo duru za kuaminika zinabaini kwamba kwa sasa baadhi ya wanajeshi wamewasili katika mji wa Koudougou, na wamepokelea kwa shangwe na vigelegele
Hakuna maoni :