MASHABIKI
wa Manchester City sasa wamekuwa mbogo na kuanza kumshambulia Meneja
wao Manuel Pellegrini baada ya Jumamosi kunyukwa 4-1 na Tottenham kwenye
Mechi ya Ligi Kuu England.Wiki mbili zilizopita Man City walikuwa kileleni mwa Ligi Kuu England baada ya kushinda Mechi zao zote 6 za Ligi Kuu England lakini sasa wamechapwa Mechi mbili mfululizo na kupokonywa uongozi wa Ligi na Mahasimu wao wakubwa Man United.
Kwa Mashabiki wengi wa Man City kuporomoka kwao ni kosa la Manuel Pellegrini na uamuzi wake wa kumpiga Benchi Kipa wao Joe Hart na kumchezesha walipochapwa 4 na Spurs haukupokelewa vyema.
Baadhi ya Mashabiki hao wamediriki hata kudai Pellegrini ni Meneja wa kawaida tu na hastahili kuongoza Timu yao yenye Wachezaji wenye hadhi ya Kisupastaa.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA/MATOKEO:
**Saa za Bongo
Jumamosi Septemba 2
Tottenham 4 Man City 1
Leicester 2 Arsenal 5
Liverpool 3 Aston Villa 2
Man United 3 Sunderland 0
Southampton 3 Swansea 1
Stoke 2 Bournemouth 1
West Ham 2 Norwich 2
Newcastle 2 Chelsea 2
Jumapili Septemba 27
1800 Watford v Crystal Palace
Jumatatu Septemba 28
2200 West Brom v Everton

Hakuna maoni :