SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / DABI YA MANCHESTER: NI JUMAPILI OLD TRAFFORD, MAN UNITED KUIVAA CITY, NANI MBABE?




DABI-MANCHESTERJUMAPILI Jiji la Manchester huko England litazizima kwa Dabi ya 170 kati ya Mahasimu Manchester United na Manchester City katika Mechi ya Ligi Kuu England.

Hadi sasa Man United ndio wanaongoza kwa kushinda Dabi 70 huku City wakishinda 49 tu.

Msimu uliopita kwenye Mechi kama hii, ikiwa ni Dabi ya kwanza Uwanjani Old Trafford kwa Meneja wa Man United, Louis van Gaal, Man United ilishinda Bao 4-2.

Safari hii, Man City, chini ya Meneja Manuel Pellegrini, wataingia dimbani wakiwa pungufu kwa kuwakosa Mastaa wao wakubwa Majeruhi David Silva na Sergio Agüero.

Lakini City wanao Wachezaji wapya waliowanunua Msimu huu, Kevin De Bruyne na Raheem Sterling, huku Wilfried Bony akivaa viatu vya Aguero kwa kucheza kama Straika.

DABI 3 ZILIZOPITA:
-Manchester United 4 (Young, Fellaini, Mata, Smalling) Manchester City 2 (Aguero 2)
Ligi Kuu England, Aprili 2015
-Manchester City 1 (Aguero) Manchester United 0
Ligi Kuu England, Novemba 2014
-Manchester United 0 Manchester City 3 (Dzeko 2, Toure)
Ligi Kuu England, Machi 2014

Kama kawaida, Man United wataongozwa na Kepteni wao Mpiganaji Wayne Rooney, ambae ametimiza Miaka 30, akisaidiwa na Chipukizi wao wapya Memphis Depay na Anthony Martial.

Baada ya Mechi 9 za Ligi, Man City wako kileleni wakiwa na Pointi 21 wakifuatiwa na Arsenal na Man United zote zikiwa na Pointi 19 huku West Ham wakishika Nafasi ya 4 wakiwa na Pointi 17.
VIKOSI:
MANUNITED-CITY-TEAMS
REFA: Mark Clattenburg
Majeruhi:
-Man United: Young, McNair, Shaw
-Man City: Delph, Agüero, Nasri, Silva, Clichy

VIKOSI:
REFA: Mark ClattenburgBPL-STAND-OKTI23
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumamosi Oktoba 24
1700 Aston Villa v Swansea            
1700 Leicester v Crystal Palace               
1700 Norwich v West Brom             
1700 Stoke v Watford            
1700 West Ham v Chelsea     
1930 Arsenal v Everton         
Jumapili Oktoba 25

1500 Sunderland v Newcastle                  
1705 Bournemouth v Tottenham              
1705 Man United v Man City           
1915 Liverpool v Southampton 

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply