DICK ADVOCAAT AJIUZULU UMENEJA SUNDERLAND!
Dick Advocaat amejiuzulu kama Meneja wa Sunderland baada ya Timu yake kutoshinda hata Mechi 1 kwenye Ligi Kuu England Msimu huu.
Advocaat, Raia wa Holland mwenye Miaka 68, aliteuliwa kushika wadhifa wa Umeneja wa Sunderland Mwezi Machi wakati Timu ikiwa hatarini kushuka Daraja Msimu uliopita.
Baada ya kuinusuru kutoshuka Daraja, Advocaat alikuwa ndio amemaliza Mkataba wake lakini akaongeza Mkataba wa Mwaka mmoja ambao ungembakisha hadi mwishoni mwa Msimu huu wa 2015/16.
Habari za kujiuzulu kwa Advocaat baada ya Mechi 8 tu za Ligi zimethibitishwa na Mwenyekiti wa Sunderland Ellis Short ambae pia amethibitisha Kocha Mkuu, Zeljko Petrovic, anaondoka Klabuni hapo.
Jumamosi, Sunderland waliumwaga uongozi wa 2-0 na kutoka Sare 2-2 na West Ham.
Katika Kipindi cha Miaka Minne, Sunderland sasa wanasaka Meneja wao wa 6.
Mameneja wengine waliopita katika kipindi hicho ni Steve Bruce, alietimuliwa Novemba 2011, na wengine ni Martin O'Neill, Paolo di Canio, Gus Poyet na huyu wa sasa Advocaat ambae aliwahi kuziongoza Netherlands, Russia na South Korea.
Kimsimamo kwenye Ligi Kuu England, Sunderland wako Nafasi ya 19, wakiwa na Pointi 3 tu sawa na Timu ya mkiani Newcastle.
Tagged with: MICHEZO
Hakuna maoni :