Serikali ya Afrika Kusini imesema
italipa fidia kwa familia za wafanyakazi wa mgodini waliouawa wakati wa
kuzuka kwa mgogoro wa Marikana mwaka 2012.
Taarifa za kina kuhusu malipo zitatolewa na jopo huru linaloongozwa na jaji, Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma ameeleza.Polisi waliwafyatulia risasi wafanyakazi 34 wa mgodi katika machimbo ya Lonmin, wakidai kuwa walikuwa wakijihami.
Kwa upande wa familia, wakili wao ameripotiwa kuunga mkono tangazo la Zuma.
Vyama vya upinzani vimetaka hoja hiyo ifikishwe bungeni ijadiliwe ili waweze kupima na kutenda haki kwa familia hizo.
Hakuna maoni :