SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / ENGLAND-BIGI MECHI WIKIENDI-DABI YA MERSEYSIDE EVERTON v LIVERPOOL, ARSENAL v MAN UNITED!





MERSEYSIDE-DABIWIKIENDI hii Ligi Kuu England inaingia Mechi zake za 8 za Msimu wa 2015/15 na Bigi Mechi ni Jumapili ambapo ipo Dabi ya Merseyside, kati ya Everton na Liverpool, na pia mtanange kati ya Arsenal na Vinara wa Ligi Manchester United.
Lakini Jumamosi zipo Mechi 7 ikiwemo ile ya Mabingwa Watetezi Chelsea kucheza na BPL-STAND-OCT1Southampton Uwanjani Stamford Bridge huku Wadau wakikazia nini kitamkuta Jose Mourinho baada ya Timu yake Chelsea kuanza vibaya utetezi wa Ubingwa wao na kujikuta wako Nafasi ya 14 wakiwa na Pointi 8 zikiwa Pointi 8 nyuma ya Vinara Man United.
Kibaya zaidi ni kufungwa kwa Chelsea huko Ureno Bao 2-1 Juzi Jumanne na FC Porto kwenye Mechi ya Kundi lao la UEFA CHAMPIONZ LIGI na hii imezidisha presha kwa Mabingwa hao.
Hiyo hiyo Jumamosi, Man City wako kwao Etihad kucheza na Newcastle huku wao pia wakikodolewa mimacho baada ya kuanza vyema Ligi kwa kushinda Mechi 5 mfululizo wakipaa kileleni na kisha kuporomoka kwa kufungwa Mechi mbili zilizopita.
Jumapili Mechi ya kwanza ni huko Goodison Park Jijini Liverpool, ikiwa ni Dabi ya Merseyside, inayozikutanisha Wenyeji Everton na Mahasimu wao wa Jadi Liverpool.
Baada ya Dabi hii zipo Mechi mbili zinazoanza muda sawa kati ya Swansea na Tottenham lakini jicho litakuwa huko Emirates kwenye mtanange mkali kati ya Arsenal na Manchester United.
ARSENALvMANUNITED-LOGO-SH
Baada ya Mechi hizi za Wikiendi hii, Ligi Kuu England itapumzika kupisha Mechi za Kimataifa na kurudi tena hapo Oktoba 17.
LIGI KUU ENGLAND                                                                                       
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumamosi Oktoba 3
1445 Crystal Palace v West Brom            
1700 Aston Villa v Stoke                 
1700 Bournemouth v Watford                  
1700 Man City v Newcastle             
1700 Norwich v Leicester                
1700 Sunderland v West Ham         
1930 Chelsea v Southampton         
Jumapili Oktoba 4
1530 Everton v Liverpool                
1800 Arsenal v Man United             
1800 Swansea v Tottenham  

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply