
Mashitaka haya yanakuja mara tu baada ya Mreno huyo kuadhibiwa na FA kwa kupigwa Faini Pauni 50,000 na Kufungiwa Mechi 1 asikanyage Uwanjani lakini Kifungo hiki kimesimama kwa Mwaka mmoja hadi Mwakani Oktoba 13 ili kuangalia mwenendo wake.
Kosa hili la sasa linatokana na madai ya kitendo cha Mourinho wakati wa Mechi na West Ham cha kutaka kwenda kwenye Vyumba vya Marefa ili kuongea na Refa Jon Moss wakati wa Haftaimu huku Timu yake ikiwa nyuma kwa Bao 1-0, kwa Bao la Penati, na pia ikiwa tayari imepewa Kadi Nyekundu 2, moja kwa Mchezaji wao Nemanja Matic na nyingine kwa Msaidizi wa Mourinho, Silvino Luoro.
Kitendo hicho kilimfanya Refa Jon Moss ampe Mourinho Kadi Nyekundu na Kipindi cha Pili chote Mourinho alikaa Jukwaa la Watazamaji huko Upton Park akiangalia Chelsea yake ikifungwa 2-1 na West Ham.
Mbali ya Shitaka kwa Mourinho, Chelsea pia inakabiliwa na Faini ya Pauni 25,000 kwa zaidi ya 5 Wachezaji wake kupewa Kadi za Njano katika Mechi hiyo.
Wachezaji wa Chelsea waliopewa Kadi za Njano ni Matic, Kadi 2, na wengine ni Cesar Azpilicueta, Willian, Cesc Fabregas, John Mikel Obi na Diego Costa.
Pia Klabu zote mbili, Chelsea na West Ham, zimepewa hadi Oktoba 29 kujibu Mashitaka ya kushindwa kudhibiti Wachezaji wao.
Hakuna maoni :