MSALA! Kuna madai mazito yanayosema kuwa nyota wa filamu Bongo, Kajala
Masanja ambaye alizaa na ‘prodyuza’ mkali wa muziki wa kizazi kipya,
Paul Matthyssen ‘P Funk’ anamharibu mtoto wao anayefahamika kwa jina la
Paula.
Chanzo ambacho pia ni rafiki wa karibu wa familia ya bosi huyo wa Bongo
Records, kinasema wazazi hao hivi sasa wako katika mvutano mkubwa
kutokana na kinachodaiwa kuwa mabadiliko ya tabia ya binti huyo mwenye
umri wa miaka 13, anayesoma kidato cha kwanza katika shule moja iliyopo
nje ya Jiji la Dar es Salaam.
Inadaiwa kuwa awali P Funk alikuwa akiishi na bintiye huyo, lakini
Kajala hakukubaliana na suala hilo, hivyo akatumia mbinu alizojua na
kufanikiwa kumchukua. Kwa ushauri wa marafiki zake, mtayarishaji huyo
mtata, aliamua kumuachia mzazi mwenziye amlee, lakini kwa uangalizi wa
karibu.
Baadaye, inadaiwa P Funk alianza kubaini mabadiliko kwa mwanaye, ikiwemo
kujichanganya na makundi ya wasanii akiwa ameongozana na mama yake,
kitu ambacho hakukipenda.
“Wakati anaishi kwa baba yake, Paula alikuwa na uwezo mzuri tu darasani,
lakini sasa hivi, anavurunda kutokana na tabia anazofundishwa na mama
yake, maana kila mahali alipo Kajala na huyo binti yupo, kwenye vikao na
wasanii wa Bongo muvi, wakati mwingine usiku,” kilisema chanzo hicho.
Gazeti hili lilimtafuta P Funk ili kusikia kauli yake kuhusiana na suala
hilo, lakini licha ya kukiri kuwepo kwa tofauti kati yake na mzazi
mwenzake juu ya malezi ya mtoto wao, alikataa kuingia kwa undani zaidi,
akidai kuwa bize na kazi.
“Yule ni binti yangu, siwezi kuona anaharibikiwa na mimi nikakaa kimya,
lazima nikemee, kwa hiyo utofauti upo, lakini kwa sasa sina nafasi ya
kulizungumzia hilo,” alisema P- Funk.Risasi Mchanganyiko lilijaribu
kuwasiliana na Kajala, lakini juhudi zake hazikuzaa matunda.
Chanzo:GPL
Quote:
What we have, what we wish we had - ambitions fulfilled, ambitions
disappointed, investments won, investments lost, elections won,
elections lost - these things may occupy our attention, but they do not
define us.
By Mitt Romney
Tagged with: BURUDANI
Hakuna maoni :