Muuza nyago maarufu Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’.
Hamida Hassan na Gladness Mallya
AIBU jamani! Muuza nyago maarufu Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’
ametia aibu baada ya kunaswa laivu hotelini akifanya yake na wanaume
wawili tofauti, Ijumaa Wikienda linaripoti.
Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na Masogange, tukio hilo lilijiri katika
Hoteli ya Lamada iliyopo Mbezi-Beach jijini Dar hivi karibuni baada ya
mrembo huyo kutua Bongo akitokea nchini Afrika Kusini ‘Sauz’ kwenye
makao yake yasiyo wazi.
Akiwa na mmoja kati ya midume hiyo.
Katika picha za tukio hilo, Masogange, akiwa kwenye vazi moja na kwa
nyakati tofauti, alikuwa akijiachia kimahaba na wanaume hao, mmoja
akitajwa kuwa ni raia wa Uganda.
“Yaani unaambiwa Masogange alikuwa na wanaume hao wawili tofauti bila
kujali ataelewekaje… da! Jamani hawa dada zetu nao,” kilisema chanzo
hicho.
Baada ya kubwagiwa ‘ubuyu’ huo na picha kutufikia, wanahabari wetu
walimwendea hewani Masogange ili atolee ufafanuzi tukio hilo lakini
hakupokea simu.
Hata hivyo, waandishi wetu hawakukata tamaa, walimtumia ujumbe mfupi kwa njia ya simu lakini pia hakujibu.
Source:Global Publishers
Hakuna maoni :