SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / MKWASA: SI KAMA DAR ES SALAAM, TUTABADILI AINA YA UCHEZAJI




Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesema watabadili aina ya uchezaji katika kikosi chake wakati wakiivaa Malawi, kesho.
Mkwasa amesema anaamini Malawi hawatacheza kama walivyocheza Dar es Salaam, hivyo Taifa Stars lazima ibadili uchezaji.

Stars inaivaa Malawi katika mechi ya pili kuwania kucheza Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka 2018.

“Tunajua mechi itakuwa ngumu, tumekuja hapa kwa ajili ya kupambana. Tutafanya kila linawezekana na kamwe hatuwezi kutumia mbinu za Dar es Salaam.


“Uchezaji wa Dar es Salaam tukiwa nyumbani lazima uwe tofauti na ugenini,” alisema Mkwasa.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply