NAAM. Sasa Afrika Kusini wanajua kuna mchezaji anaitwa Mrisho Khalfan Ngassa (pichani kulia) yuko Bethelehem na mashabiki jana wamembatiza jina ‘Messi’, wakimfananisha Mwanasoka Bora wa Ulaya, Muargentina Lionel Messi.
Ngassa
jana amewalamba vyenga wacheaji wa Bidvest Wits na kumpasia Danny
Venter kufunga bao pekee dakika ya 72 Free State Stars ikishinda 1-0 na
kutinga Robo Fainali za michuano ya Kombe la Telkom Knockout Afrika
Kusini.
Katika
mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Goble Park mjini Bathelehem yalipo
makao makuu ya Free State, Ngassa alicheza soka ya nguvu kiasi cha
mashabiki kumuimba ‘Messi Messi’ kila anapokuwa na mpira.
Akizungumza
na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE leo, Ngassa amesema sasa anafurahia
maisha Afrika Kusini na jana mashabiki wamempa jina Messi.
“Baada
ya mechi viongozi wa Bidvest walinifuata na kuchukua namba yangu,
wanaonyesha nia ya kunihitaji. Kwa kweli sasa ninacheza na watu sasa
wanajua kuna mtu anaitwa Ngassa,”amesema.
Ngassa
anapanda ndege mchana wa leo kurejea Dar es Salaama mara moja kujiunga
na kambi ya timu ya taifa, Taifa Stars kwa maandalizi ya michezo ya
kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Malawi.
Stars: Diakite, Mashego, Sankara, Chakoroma/Mohomi dk28’, Rakoti, Thlone, Ngasa, Masehe, Venter, Fileccia na Ngcobo/Sekola dk46.
Wits:
Josephs, Allie, Hlatshwayo, Mkhwanazi, Bhasera, Pelembe/Motshwari dk80,
Shongwe, Ntshangase, Klate, Vilakazi/Kadi dk61 na Lupeta/Mahlambi dk60.
Tagged with: MICHEZO
Hakuna maoni :