Shirikisho la soka duniani Fifa
limemsimamisha kazi kwa mda rais wake Sepp Blatter ,katibu wake Jerome
Valcke na makamu wa rais Michel Platini kwa siku tisini.
Adhabu hiyo ilitolewa na kamati ya maadili katika shirikisho hilo.
Blatter,Valcke na rais wa UEFA Platini wanachunguzwa na kamati hiyo kuhusu madai ya ufisadi.
"Uamuzi huo unatokana na uchunguzi unaofanywa na kamati ya maadili katika shirikisho hilo'',ilisema taarifa.
Watatu hao wamepigwa marufuku kushiriki katika michezo yoyote ya kandanda kwa mda huo.
Anatuhumiwa kwa kutia saini kandarasi isiyokuwa na umuhimu wowote kwa FIFA mbali na kutoa malipo kwa rais wa shirikisho la UEFA Michel Platini kinyume na matakwa ya shirikisho hilo.
Platini pia amesimamishwa kazi.
Kamati ya maadili pia ilianzisha uchunguzi dhidi ya Platini kuhusu malipo hayo ya Yuro milioni 2 ambayo yalifanywa miaka minane baada ya PLatini kumfanyia kazi Blatter.
Valcke tayari alikuwa katika likizo kufuatia taarifa ilioandikwa katika gazeti moja kwamba anahusika na kashfa ya kutaka kujinufaisha na tiketi za kombe la dunia.
Hakuna maoni :