Klabu ya African Sports imesema haina fedha za
kuwasafirisha wachezaji wake kutoka Mbeya kwenda Tanga kupiga kura kisha
kurejea tena mkoani humo kucheza na Prisons Alhamisi ijayo.
Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani
unafanyika kote nchini kesho Jumapili ikiwa ni fursa ya wananchi wa Tanzania
kuchagua viongozi wao.
Makamu Mwenyekiti wa African Sports, Ahmed
Bozinia amesema kuwa, kikosi chao kipo Mbeya kikisubiri mechi dhidi ya Prisons,
Alhamisi ijayo na wachezaji hawatapiga kura kesho.
“Wachezaji wetu walijiandikisha Tanga, lakini
hatuna bajeti ya kwenda Tanga kupiga kura na kurudi Mbeya tena kwa ajili ya
mechi. Tumeona ni heri kupoteza upande mmoja kwa ajili ya masilahi ya upande
mwingine.
Hakuna maoni :