SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / AMINI USIAMINI, JUMAMOSI BIGI MECHI VINARA WA LIGI LEICESTER NA MAN UNITED, LEICESTER KUITWANGA TENA MAN 5?


LEICESTER-MANUNITEDMSIMU uliopita, Manchester United waliongoza 3-1 huko King Power Stadium na kujikuta wakitandikwa 5-3 na Leicester City katika Mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Septemba BPL-STENDI-NOV2721, 2014 na Jumamosi Timu hizi zinakutana Uwanja huo huo.


Safari hii, Leicester City, ndio Vinara wa Ligi Kuu England, wakiwa Pointi 1 mbele ya Man United iliyo Nafasi ya Pili.

Mwaka Jana, Straika wa Leicester, Jamie Vardy, alifunga Bao lake la kwanza kwenye Ligi na kutengeneza zote 4 walipoifunga Man United 5-3, na safari hi indie anaongoza kuwa Mfungaji Bora wa Ligi.


Safari hii, Leicester wapo chini ya Kocha Claudio Ranieri ambae mara ya mwisho alifukuzwa akiwa Kocha wa Greece baada ya Nchi hiyo kufungwa na Vibonde wa Ulaya Faroe Islands.



Ranieri, akisifika kama ‘Tinkerman’, yaani mbadilisha Kikosi kila kukicha, na mlolongo wa Klabu/Nchi alizowahi kufundisha [Na pia kutimuliwa]:
1986–1987   Lametini
1987–1988   Puteolana
1988–1991   Cagliari
1991–1993   Napoli
1993–1997   Fiorentina
1997–1999   Valencia
1999–2000   Atlético Madrid
2000–2004   Chelsea
2004–2005   Valencia
2007  Parma
2007–2009   Juventus
2009–2011   Roma
2011–2012   Inter Milan
2012–2014   Monaco
2014  Greece
2015– Leicester City

Je Man United watakubali kupigwa 5 na Leicester kubaki kileleni?
Hilo ndilo swali la Wachambuzi wengi huko England lakini wengi, safari hii, hawaipi nafasi Leicester.

Wengi, wanadai, udhaifu wa Man United kwenye Difensi, ukichangiwa na Penati tata 2 na Goli tata 1, ndio uliwapa Leicester ushindi huo
.
Wengi wa Wachambuzi hao wanadai mwisho wa Leicester kuselelea kileleni unaanza sasa kwani kati ya Jumamosi na Mwaka mpya Mechi zao ni dhidi ya Vigogo ambao ni Man United, Swansea, Chelsea, Everton, Liverpool na Man City.

KWA LISTI HII, LEICESTER ATANUSURIKA KWELI?
LIGI KUU ENGLAND:
**Saa za Bongo
Jumamosi Novemba 28
1800 Aston Villa v Watford             
1800 Bournemouth v Everton         
1800 Crystal Palace v Newcastle             
1800 Man City v Southampton                 
1800 Sunderland v Stoke                
2030 Leicester v Man United               
Jumapili Novemba 29
1500 Tottenham v Chelsea             
1705 West Ham v West Brom         
1915 Liverpool v Swansea              
1915 Norwich v Arsenal

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply