Simba imerejea
mazoezini na kuanza kujifua kwa ajili ya Ligi Kuu Bara. Hiyo ilikuwa ni baada
ya mapumziko ya takribani siku kumi.
Mazoezi hayo ya Simba
yamefanyika kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Ndiyo mazoezi ya kwanza Simba inafanya bila ya kuwa na kocha wake msaidizi, Selemani Matola aliyeamua kubwaga manyanga.
Mazoezi
yalihudhuriwa na Kocha Mkuu Dylan Kerr lakini zaidi yaliongozwa na
kocha wa makipa, Iddi Salum raia wa Kenya. Lakini baadaye, Kerr naye
aliingia mtamboni.
Hata hivyo, Simba inawakosa nyota wake wengi, walio katika kikosi cha Taifa Stars, Kilimanjaro Stars pia The Cranes ya Uganda.

Hakuna maoni :