Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo imemteua aliyekuwa naibu
Spika wa Bunge la 10 Job Ndugai, kuwa mwakilishi wa chama hicho
atakayegombea nafasi ya uspika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, ambaye atapigiwa kura na wabunge wa hapo kesho kuwania nafasi
hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya chama hicho iliyotolewa na Dodoma kupitia
Katibu wa Itikadi na Unezi, Nape Nauye, amesema Dkt. Tulia Mwansasu na
Mbunge wa Afrika Mashariki, Abdulla Ally Mwinyi waliamua kujitoa katika
nafasi hiyo hivyo kumpa nafasi Job Ndugai kupita bila kupingwa.
Tagged with: SIASA


Hakuna maoni :