Kamati Kuu CCM imewapitisha Job Ndugai, Abdullah Ali Mwinyi na Dr. Tulia
Ackson Mwansasu kugombea nafasi ya Uspika wa Bunge la 11.
Majina hayo yamepenya kutoka katika orodha ya majina 21, miongoni mwao
akiwemo Spika wa Bunge la 9, Samuel Sitta, Dkt. Didas Masaburi ambaye
alitangaza kujitoa katika dakika za mwisho, Dkt Kalokola na wengineo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jioni ya leo baada ya kikao cha Kamati
Kuu kilichoongozwa na mwenyekiti wake Dkt Jakaya Kikwete mjini Dodoma,
jina moja kati ya hayo matatu litatangazwa kesho Jumatatu ikiwa ni
pamoja na jina la mgombea wa nafasi ya Naibu Spika.
Katika waliopitishwa:
Job Ndugai ni mbunge mteule jimbo la Kongwa Dodoma na pia alikuwa Naibu Spika wa Bunge lililopita.
Dkt Tulia Ackson ni Naibu Mwanasheria mkuu wa serikali, pia alikuwa ni
mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba akitokea taasisi za elimu ya juu.
Amekuwa mhadhiri wa sheria katika kitivo (sasa shule) cha sheria chuo
kikuu cha Dar es salaam.
Abdullah Mwinyi ni mtoto wa Rais mstaafu Al Hajj Aly Hassan Mwinyi na ni mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki.
Home
/
SIASA
/
Breaking News:CCM Yapitisha Majina Matatu ya Wagombea Uspika......Samwel Siita, Emmanuel Nchimbi Out!!!
Breaking News:CCM Yapitisha Majina Matatu ya Wagombea Uspika......Samwel Siita, Emmanuel Nchimbi Out!!!
Tagged with: SIASA


Hakuna maoni :