Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeanza jana mjini
Dodoma na moto ambao wengi waliutabiri huku harufu ya ushabiki wa vyama
ikitawala.
Katika zoezi la kumtafuta Spika wa Bunge hilo lililotanguliwa na maswali
na majibu kwa wagombea nane waliojitokeza, Mgombea Uspika kupitia
Chadema, Goodluck ole Medeye alikwaruzana kimtazamo na mbunge wa jimbo
la Mtama, Nape Nnauye.
Swali la Nape lililokuwa kati ya maswali matatu aliyoulizwa Ole Medeye
lilionekana kumuudhi mgombea huyo. Nape alimtaka Ole aeleze kama ameacha
tabia ya ubaguzi kwa madai kuwa Godbless Lema aliwahi kumtuhumu kuwa ni
mbaguzi.
Ingawa Mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo, Andrew Chenge alikataa swali
hilo lisijibiwe akieleza kuwa halikuwa swali, Ole Medeye alihitimisha
kwa kumueleza Nape alichokuwa nacho moyoni ingawa hakumtaja jina.
“Kuna mbunge hapa aliniuliza swali ambalo kwa
lugha za kibunge tunaliita ni swali la kuudhi. Mbunge huyo nimemsamehe,
sina chuki naye kwa sababu najua kinachomsumbua ni utoto tu, akikua
ataacha,” alisema Ole Mideye.
Uchaguzi huo ulikamilika na kumuwezesha Job Ndugai kuwa spika wa Bunge hilo baada ya kupata asilimia 70 ya kura zote.
Tagged with: SIASA


Hakuna maoni :