Baada ya zoezi la kuuaga mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha
demokrasia na maendeleo (Chadema) mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo
kushindikana kutokana na jeshi la polisi mkoani Mwanza kupiga marufuku
mikusanyiko ya wanachama na wafuasi wa chama hicho kwa madai ya kuwepo
kwa ugonjwa wa kipindupindu jijini Mwanza, hatimaye viongozi wakuu wa
kitaifa wa Chadema pamoja na familia ya marehemu wameamua kwenda
mahakamani kesho kutafuta haki yao ya kisheria.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Mwanza na mwenyekiti wa Chadema taifa
Mh. Freeman Mbowe akiwa pamoja na Waziri mkuu mstaafu Mh. Fredrick
Sumaye pamoja na aliyekuwa mgombea urais kupitia chama cha demokrasia na
maendeleo (Chadema) akiungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba
ya wananchi (UKAWA) Mh. Edward Lowassa.
Naye Mchungaji Charles Lugiko ambaye ni baba wa marehemu Alphone Mawazo
amelaani kitendo cha askari polisi kwenda hadi nyumbani kwake eneo la
Nyegezi na kuwatawanya waombolezaji waliokuwa wamekusanyika nyumbani kwa
ajili ya kuuaga mwili wa marehemu Mawazo.
Alphonce Mawazo aliuawa kikatili kwa kukatwa mapanga na mashoka na watu
wasiojulikana Novemba 14 mwaka huu katika kijiji cha katoro wilayani
Geita.
Home
/
SIASA
/
Chadema Kufungua Kesi Kupinga Agizo la Polisi Kuzuia Kuagwa Mwili wa Alphonce Mawazo.
Chadema Kufungua Kesi Kupinga Agizo la Polisi Kuzuia Kuagwa Mwili wa Alphonce Mawazo.
Tagged with: SIASA


Hakuna maoni :