Timu ya taifa ya Jamuhuri ya
Ireland,imetinga katika fainali za michuano ya Ulaya baada ya kupata
ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya Bosnia-Herzegovina.
Jamuhuri ya Ireland imesubiri kwa miaka sita kuweza kupata nafasi hiyo ambapo mwaka 2009 walikosa nafasi hiyo dakika za mwisho baada ya kufungwa na ufaransa bao la utata lilofungwa kwa mkono na mshambuliaji Thierry Henry'
Katika mchezo wa kwanza timu hizi zilikwenda sare ya kufungana bao 1-1 hivyo Ireland imepita kwa jumla ya mabao 3-1.
Leo kutachezwa michezo miwili ya mwisho itakayotoa timu mbili za mwisho zitakazoshiriki michuano ya Euro hapo mwakani nchini Ufaransa.
Slovenia itakua mwenyeji wa Ukraine katika mchezo wa kwanza Ukraine iliishinda Slovenia kwa mabao 2-0.
Denmark itakipiga na Sweden huku mchezo wa kwanza Sweden iliitambia Denmark kwa kuwafunga mabao 2-1.


Hakuna maoni :