Katika hali isiyo kuwa ya kawaida Chama cha Demokrasia na Maendeleo
mkoani Shinyanga leo kimedai kwamba Jeshi la Polisi mkoani humo
limefanya maandamano ya Chadema bila kujijua.
Kwa mujibu wa baadhi ya viongozi wa chama hicho walidai kupokea taarifa
kutoka kwa uongozi wa juu wa chama hicho ukiwataka kufanya maandamano
leo nchi nzima ya kupinga ushindi wa Dkt. John Pombe Magufuli kwa madai
kuwa demokrasia imebakwa katika mchakato mzima wa uchaguzi mkuu
uliofanyika tarehe 25 oktoba 2015.
Katibu wa Chadema wilaya ya Shinyanga mjini George Kitalama amesema
kwamba chama hicho kimefanikiwa kufanya maandamano kupitia jeshi la
polisi lililozunguka mji mzima kuwasaka wanachama wa chadema na
kuambulia patupu.
“Tulipanga kufanya maandamano leo Novemba 03,2015 mji mzima wa Shinyanga
lakini polisi ndiyo wamejitokeza kufanya maandamano wakiwa na magari
yao kila mtaa.”Alisema Kitalama.
Kufuatia taarifa ya Chadema kutaka kufanya maandamano katika maeneo
mbalimbali nchini Askari wa Jeshi la Polisi wamekuwa katika misururu ya
magari yakiwemo ya maji ya kuwasha wakizunguka kuwasaka waandamanaji
kutoka chama hicho ambao hawakufanikiwa kufanya maandamano hayo.
Jijini Dares salaam Askari Polisi wakiwa kwenye punda na wengine wa
doria wameonekana katika maeneo mbalimbali ikiwemo maeneo nyeti na yenye
ofisi nyingi za Serikali ikiwemo Posta.
Home
/
MATUKIO
/
Katika Hali Isiyo ya Kawaida...Chadema ‘Wajigamba’ Kuwafanyisha Polisi Maandamano Bila Kujijua
Katika Hali Isiyo ya Kawaida...Chadema ‘Wajigamba’ Kuwafanyisha Polisi Maandamano Bila Kujijua
Tagged with: MATUKIO
Hakuna maoni :