• Manchester City (4-2-3-1): Hart 7, Maffeo 6.5, Stones 7 (Adarabioyo 60, 6)...

  • SALVATORY EDWARD Kiungo wa zamani wa timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kide...

  • Baada ya kikosi cha Mwadui FC kuchapwa kwa bao 1-0 katika mechi yao ya Lig...

  • Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeweka bayana kuwa, lipo kwenye mpango wa ...

SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / Kauli ya Uongozi wa Diamond Baada ya Ali Kiba Kudai Diamond Ametumia Fedha Kupata Tuzo za Afrima


Baada ya Alikiba kupost ujumbe katika Instagram akidai kuwepo na mambo yanayoendelea nyuma ya pazia kwenye muziki wake na wengi kutafsiri amelalamikia kukosa tuzo za Afrima, uongozi wa Diamond aliyeshinda tuzo tatu umezungumza.Akizungumza katika pindi cha XXL cha Clouds FM, mmoja kati ya mameneja wa Diamond, Babu Tale alisema walisikitishwa na ujumbe huo.“Mimi naona asiyekubali kushindwa sio mshindani,” alisema. “Hata sisi tumeshawahi kuingia kwenye tuzo ambazo na yeye aliongea maneno hayo alikuwepo na akashinda na hakuna mtu yeyote aliongea sijui mmenunua tuzo. Mimi nilijua mashabiki ndio wanaongea mpaka msanii anapost kitu kama kile nikahisi labda kuna mtu amehack akaunti yake. Kwahiyo nilivyoona vile nikamhukumu sio mshindani,” alisema Tale.

Hata hivyo Tale alisema baada ya kufuta kauli hiyo na kuzungumzia kauli hiyo aligundua huenda alishinikizwa na mashabiki wake.

Lakini baadaye baada ya kuona ameongea vizuri, nikagundua sometimes mtu anaweza kupaniki kwa ajili ya mashabiki wanaoongea. Lakini mwisho wa siku tunatakiwa tukae meza moja ili tusukume muziki wetu wa Tanzania. Tukiangalia line up ya muziki wa Afrika sasa hivi tupo namba mbili, tunakwenda kwenye namba 1,” aliongeza.

Hata huvyo Alikiba aliifuta post hiyo na kudai kuwa hakuandika kwa sababu alikosa tuzo.

«
Next
Lipumba Ameibuka Tena, Amemtaka Rais John Magufuli Kuiamulia Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Kumtangaza Maalim Seif Kuwa Rais
»
Previous
Aliyeokolewa Mgodini Amuulizia LOWASSA Kama alifanikiwa Kushinda Urais

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply