SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / KIMATAIFA KIRAFIKI: LINGARD AITWA KWA MARA YA KWANZA KIKOSINI ENGLAND KUIVAA FRANCE!


MANUNITED-LINGARDFOWADI wa Manchester United Jesse Lingard ameiwa kwenye Kikosi cha England ambacho kitaivaa France Uwanjani Wembley Jijini London Jumanne Usiku katika Mechi ya Kirafiki.

Lingard, mwenye Miaka 22, amekichezea Kikosi cha Vijana wa England cha U-21 mara 11 lakini hii ni mara ya kwanza kabisa kuitwa kwenye Kikosi cha Kwanza cha England.
 
Lingard ameitwa Kikosini wakati England ikikabiliwa na Majeruhi baada ya Mchezaji mwenzake wa Man United, Michael Carrick, kuumia walipofungwa Ijumaa na Spain na pia Fowadi wa Leicester, Jamie Vardy, kuwa pia na maumivu na kujiondoa Kikosini.

Lingard alipoingizwa toka Benchi dhidi ya Scotland hapo Agosti 2013 na ni Mchezaji aliekulia Kisoka kwenye Chuo cha Soka cha Man United na kuichezea Timu ya Kwanza yake mara 7 na pia kucheza kwa Mkopo na Klabu za Leicester, Birmingham, Brighton na Derby.

Novemba 7, Lingard aliifungia Man United Bao lake la kwanza wakati wanaifunga West Brom Bao 2-0 kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
KIMATAIFA KIRAFIKI
Ratiba:
*Saa za Bongo
Jumanne Novemba 17
Tuesday 17 Nov 2015         
3:00   Italy v Poland                   
3:00   Lebanon v New Zealand              
14:00 Macedonia v Lebanon                 
18:00 Russia v Croatia               
19:00 Estonia v Saint Kitts And Nevis             
19:00 Azerbaijan v Moldova                 
20:15 Turkey v Greece               
21:30 Luxembourg v Portugal               
21:45 Austria v Switzerland                  
21:45 Poland v Czech Republic             
21:45 Slovakia v Iceland            
21:45 Belgium v Spain               
22:00 England v France              
22:45 Germany v Netherlands              
22:45 Italy v Romania

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply