SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / MAJEGWA: NIKIPATA NAFASI SIMBA, KWANGU LITAKUWA NI JAMBO LA BAHATI, SITALIFANYIA MCHEZO


Kiungo mshambuliaji, Brian Majegwa amesema kamwe hatajivunga kama akipata nafasi ya kucheza Simba.


Majegwa ambaye bado ana mgogoro na Azam FC, kwa mara nyingine amesema angependa kumalizana na Azam FC ili aondoka.

“Mpira una mzunguko, sina maana nataka kugombana na Azam FC. Ninataka kuondoka niende na maisha yangu,” alisema.

Alipoulizwa kama akipata nafasi ya kuitumikia Simba ambayo sasa anafanya nayo mazoezi baada ya kuomba, akasema:

“Nafasi ya kuitumikia Simba, kwangu litakuwa jambo bora kabisa. Nitafurahi na kufanya kazi hiyo kwa juhudi zote ili nifanikiwe.”

Taratibu suala la Majegwa linaanza kuchukua vichwa vya habari katika vyombo mbalimbali vya habari kwa Azam FC imesema Mganda huyo bado mali yake na ilimpeleka kwa mkopo KCCA ua Uganda.

Lakini Majegwa anasema hajalipwa mshahara wa miezi mitatu hadi sasa. Hivyo angependa kupata haki yake, lakini pia apewe nafasi ya kuondoka akiamini mkataba umeishavunjika.


Kuna taarifa nyingine kwamba Simba imeshamalizana naye, lakini viongozi wake wamekuwa wakisisitiza, bado!

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply