Mwanasheria mkuu wa serikali, George Masaju amepinga hoja zilizoibuliwa
na UKAWA kuhusu uhalali wa rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar,
Dkt Shein, kuhudhuria kwenye uzinduzi wa Bunge.
Masaju ametumia ibara ya 102 ya katiba ya jamhuri ya muungano wa
Tanzania kupangua hoja hizo ambayo inaeleza kuwa, kutakuwa na serikali
ya Zanzibar itakayo julikana kama serikali ya mapinduzi ya Zanzibar
ambayo itakuwa na mamlaka katika Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo mambo
ya muungano kwa mujibu wa masharti ya katiba hii.
Pia ametumia ibara ya 103 ibara ndogo ya kwanza ya katiba ya jamhuri
inayosema kuwa, kutakuwa na kiongozi wa serikali ya mapinduzi ya
Zanzibar ambae ndiye atakuwa rais wa Zanzibar na mkuu wa serikali ya
mapinduzi ya Zanzibar na vilevile mwenyekiti wa baraza la mapinduzi.
Baada ya Ibara hizo, akajielekeza kwenye katiba ya Zanzibar ya mwaka
1984 katika Ibara yake ya 26 ambayo inasema, kutakuwa na rais wa
Zanzibar ambae atakuwa mkuu wa nchi ya Zanzibar, kiongozi wa serikali ya
mapinduzi ya Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi.
Hali kadhalika akanukuu Ibara ya 27 ambayo inaeleza namna rais wa
Zanzibar atakavyo patikana ambayo inasema kwamba, rais atachaguliwa
kufuatana na katiba hii na kwa mujibu wa sheria yoyote itakayotungwa na
baraza la wawakilishi kuhusu uchaguzi wa rais na mwenyekiti wa baraza la
mapinduzi na uchaguzi wa rais utafanyika katika tarehe itakayowekwa na
tume ya uchaguzi (ikiwa na maana ya ZEC).
Aidha, alinukuu Ibara ya 28 (a) ya katiba ya Zanzibar ambayo inaeleza
kwamba, kufuatana na katiba hii, mtu ataendelea kuwa rais mpaka:
a) Rais anaefata ale kiapo cha kuwa rais
Baada ya hoja hizo akahitimisha kwa kusema, kwa kuwa tayari tume ya
uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imefuta uchaguzi, na kwa kuwa tayari tume
hiyo imetangaza tarehe ya kufanyika uchaguzi mkuu mwingine visiwani
Zanzibar, na kwa kuwa hakuna mtu yeyote alieapa kiapo cha urais tofauti
na rais wa sasa wa Zanzibar, Dkt Shein. Hivyo Dkt Shein anatambulika
kama rais wa Zanzibar na ana uhalali wote wa kuhudhuria katika uzinduzi
wa Bunge la 11.
Home
/
SIASA
/
Mwanasheria Mkuu Apinga Hoja za UKAWA...Asema Dr. Shein ni Rais Halali wa Zanzibar na atahudhuria Uzinduzi wa Bunge la 11
Mwanasheria Mkuu Apinga Hoja za UKAWA...Asema Dr. Shein ni Rais Halali wa Zanzibar na atahudhuria Uzinduzi wa Bunge la 11

Tagged with: SIASA
Hakuna maoni :