BEKI
wa Manchester United Marcos Rojo amepasua ukweli kuhusu uhusiano wake
na Meneja Louis van Gaal baada ya kuwepo ripoti kuwa hali si nzuri kati
yao.Kabla Msimu huu kuanza, Mchezaji huyo wa Argentina alichelewa kujiunga na wenzake huko USA wakati wa Mazoezi ya kabla Msimu kuanza kwa sababu ya matatizo ya Pasipoti yake.

Kuchelewa kwake kulimfanya aichezee Man United Mechi 2 tu kati ya 13 za kwanza za Msimu mpya na hilo kuleta minong’ono kuwa ataondoka Mwaka mmoja tu tangu atue hapo kutokea Sporting Lisbon ya Portugal.
Lakini baada ya hapo Rojo akaichezea Mechi zao zote 6 akiimudu nafasi ya Fulbeki wa Kushoto na kumfanya hata Van Gaal mwenyewe asifie uchezaji wake.
Alipohojiwa na ESPN, kama ana uhusiano mzuri na Van Gaal, Rojo alijibu: “Ni kawaida tu kama wa Kocha mwingine. Simuulizi kwa nini ananipanga nicheze Mechi na hivyo sina haki ya kumuuliza kwa nini hanipangi. Hiyo ndio hali halisi.”
Rojo amesisitiza Van Gaal anaamua Mchezaji gani acheze Mechi kutokana na tathmini ya Wiki nzima na kila Mtu anapaswa kukubali hilo.
Rojo alifafanua: “Ni Kocha mahiri anaetaka kila mmoja wetu awe bora. Si Kocha mbaya. Anataka mafanikio na tunapaswa kuelewa nini anataka toka kwetu.”
Hivi sasa Ligi Kuu England ipo kwenye mapumziko kupisha Mechi za Kimataifa na itarejea tena Jumamosi Novemba 21 na Mechi ya kwanza Siku hiyo ni ya Man United Ugenini na Watford.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Baada ya Mechi za Novemba 8, Ligi kusimama kupisha Mechi za Kimataifa
Jumamosi Novemba 21
1545 Watford v Man United
1800 Chelsea v Norwich
1800 Everton v Aston Villa
1800 Newcastle v Leicester
1800 Southampton v Stoke
1800 Swansea v Bournemouth
1800 West Brom v Arsenal
2030 Man City v Liverpool
Jumapili Novemba 22
1900 Tottenham v West Ham
Jumatatu Novemba 23
2300 Crystal Palace v Sunderland

Hakuna maoni :