Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Mkur, Dk
Hellen Kijo-Bisimba anatarajia kusafirishwa kwenda nchini India kwa
ajili ya matibabu zaidi.
Novemba 7, mwaka huu Dk Bisimba alipata ajali ya gari katika barabara ya
Ali Hassan Mwinyi na kuvunjika mshipa wa paja na goti sanjari na
kujeruhiwa kichwa,bega na mgongo.
Akizungumza jana akiwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya
Fahamu (MOI) ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam, Dk
Bisimba alisema kwa sasa anaendelea vizuri na kwamba anatarajiwa
kupelekwa nchini humo na watoto wake kwa matibabu zaidi.
Alisema safari yake hiyo siyo kwa sababu ya upungufu wa huduma
aliyoipata kutoka MOI bali ni kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi
wa mwili wake.
“Namshukuru Mungu naendelea vizuri. Tangu nimekuja hapa MOI,
nimesikilizwa na kuhudumiwa vizuri. Watoto wangu wanashugulikia usafiri
na siku yoyote naenda India ,”alisema.
Meneja Uhusiano MOI, Jumaa Almasi alisema kuwa Dk Bisimba bado anahitaji
uangalizi wa hali ya juu katika kipindi hiki kutokana na kupata
majeraha mengi kwenye mwili wake.
“Hali ya Dk Bisimba imevunja rekodi. Mbali na kumshughulikia sehemu
hizo mbili (paja na goti), kutokana na kuwa na kisukari na presha
tumeshindwa kulazimisha matibabu ya haraka kwa viungo vyote,” alisema.
Home
/
MATUKIO
/
Soma Hapa Walichoamua Watoto wa Dk Hellen Kijo-Bisimba Mkurugenzi wa (LHRC) Baada ya Kupata Ajali ya Gari
Soma Hapa Walichoamua Watoto wa Dk Hellen Kijo-Bisimba Mkurugenzi wa (LHRC) Baada ya Kupata Ajali ya Gari
Tagged with: MATUKIO


Hakuna maoni :