Wazanzibari wanaoishi nchini Uingereza jana walifanya maandamano wakidai
haki ya kutangazwa ushindi wa Chama Cha Wananchi (CUF) katika uchaguzi
mkuu wa Zanzibar uliofanyika Octoba 25 mwaka huu
Maandamano hayo yaliandaliwa na Jumuiya ya Zanzibar Welfare Association
(ZAWA) ambapo wazanzibari hao walitoka maeneo mbali mbali katika miji
yao na kukusanyika katika eneon la Downing Street kwenye Ofisi ya
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron na uongozi huo kukabidhi barua
yao yenye malalamiko kutaka suala la Zanzibar lishughulikiwe.
Maandamano hayo yalifanyika kwa lengo la kuongeza shindikizo kwa mamlaka
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuchukua hatua za haraka ya
kuhakikisha Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) inakamilisha kazi ya
kutangaza matokeo ya uchaguzi huo.
Zanzibar iliingia katika mkwamo wa kisiasa baada ya Mwenyekiti wa Tume
ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salum Jecha Octoba 28 kutangaza kuufuta
uchaguzi wote kwa madai kwamba ulikumbwa na matatizo mbali mbali.
Wakati jecha akitoa tangazo la kufuta matokeo bila ya kushauriana na
tume yake alikuwa tayari ameshatangaza matokeo ya kura za urais za
majimbo 31 kati ya 54 ya Zanzibar pia washindi wa nafasi za uwakilishi
na udiwani katika majimbo hayo walishatangazwa na walishakabidhiwa vyeti
vyao.
Rashid Ali ambaye ni kiongozi wa ZAWA alisema jana kuwa wamewasilishwa
barua hiyo wakiamini kwamba suala la Zanzibar litashughulikiwa ili
wananchi wa Zanzibar waweze kuendelea na maisha yao ya kawaida.
Mwakilishi wa ZAWA, Hassan Khamis alisema wameamua kupeleka barua kwenye
ofisi za waziri Mkuu wakiamini suala hilo litashughulikiwa ikiwa ni
pamoja na serikali ya Tanzania kuchukua hatua madhubuti na za haraka
kaika kushughulikia suala hilo ambalo limewaweka wazanzibari roho juu.
Home
/
SIASA
/
Wazanzibari Wanaoishi Uingereza Waandamana Wakitaka Maalim Seif Sharif Hamad Atangazwe mshindi wa Kiti cha Urais
Wazanzibari Wanaoishi Uingereza Waandamana Wakitaka Maalim Seif Sharif Hamad Atangazwe mshindi wa Kiti cha Urais
Tagged with: SIASA




Hakuna maoni :