Katika maongezi ya awali meneja wa bandari alimuhakikishia kuwa mfumo hauruhusu kontena kuibiwa lakini waziri mkuu alienda na ripoti ya ukaguzi na kumuonyesha majina ya waliopitisha makontena zaidi 2431 bila kulipiwa kodi.
Amempa muda wa masaa matatu hadi saa kumi na mbili jioni aambiwe hatua zilizochukuliwa kwa wahusika kwa sababu anawafahamu.
Katika hatua nyingine, Waziri mkuu alitembelea shirika la reli na kukuta mabilioni yametumika na miradi iliyokusudiwa haijatekelezwa.
Hakuna maoni :