MSHAMBULIAJI
wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ameingia tatu bora ya
Tuzo ya Mwanasoka Bora anayecheza soka la ndani barani Afrika.
Tovuti ya Shirikisho la Soka Afrika
imesema Samatta ameingia fainali na kipa Robert Kidiaba anayecheza naye
TP Mazembe ya DRC na Baghdad Boundjah wa Algeria na Etoile du Sahel ya
Tunisa.
Katika tuzo ya Mwanasoka Bora wa
Jumla wa Afrika, walioingia fainali ni Andre Ayew wa Ghana na Swansea
City, Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na Borussia Dortmund na Yaya
Toure wa Ivory Coast na Manchester City, anayeshikilia tuzo hiyo.
Majina
hayo yametangazwa mchana wa leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari
mjini Abuja, Nigeria na washindi watapatikana kutokana na kura
zitakazopigwa na makocha wakuu wa timu za taifa au Wakurugenzi wa Ufundi wa Vyama na mashirikisho ya soka ya nchi zote wanachama wa CAF.
Washindi watatangazwa katika usiku wa tuzo za Glo-CAF Januari 7 mwaka 2016.
Hakuna maoni :