SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / JUUKO MURISHID AIONGOZA THE CRANES KUITWANGA AMAVUBI YA NIYONZIMA NA KUBEBA UBINGWA CHALENJI


Uganda ‘The Cranes’ wameibuka mabingwa wa michuano ya Chalenji iliyomalizika leo nchini Ethiopia.

Bao la Uganda lilifungwa na Caesar Okhuti katika dakika ya 14 akiunganisha krosi safi kutoka Magharibi ya uwanja mjini Addis Ababa.
Timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars ilitolewa katika hatua ya robo fainali kwa kufungwa kwa mikwaju 4-3 ya penalti na wenyeji Ethiopia ambao waling'olewa nusu fainali kwa penalti pia na Waganda.


The Cranes wameibuka na ubingwa baada ya kuichapa Rwanda 'Amavubi' kwa bao 1-0.

Safu ya ilinzi ya Uganda ilikuwa inaongozwa na beki wa Simba, Juuko Murishid ambaye ameingoza timu hiyo kubebwa ubingwa dhidi ya Rwanda ambayo ilikuwa na kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzoma na kiungo wa Azam FC, Jean Baptiste Mugiraneza.

Licha ya Uganda kupata bao katika kipindi cha kwanza, lakini mechi hiyo ilikuwa ya upinzani mkubwa hadi mwisho.


Uganda iliyoanza michuano hiyo kwa kupoteza mechi kupoteza, inafundisha na Kocha Mserbia, Milutin Sredojevich ‘Micho’

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply