SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / KIFAA KIPYA CHA YANGA CHAANZA MAZOEZI DAR, PLUIJM ATAKA KUJIRIDHISHA, AMBEBA KWENDA NAYE TANGA


Mshambuliaji Issoufou Boubacar Garba 'Diego' tayari ameanza mazoezi na kikosi cha Yanga.


Diego raia wa Niger ametua nchini jana, leo ameanza mazoezi akiwa na Yanga chini ya Kocha Hans van der Pluijm.

Katika mazoezi ya Yanga yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Polisi jijini Dar es Salaam, Diego alipata nafasi ya kuonyesha vitu kadhaa.

Hata hivyo, Kocha Pluijm ameamua kumbeba mshambuliaji huyo kwenda naye Tanga ambako atapata nafasi zaidi ya kumuangalia kabla ya kupitisha uamuzi wa kumsajili au la.

Yanga inaondoka kesho kwenda Tanga ambako itakua na mechi mbili za Ligi Kuu Bara ikianza na Mgambo Shooting Jumamosi kabla ya kuivaa African Sports katika mechi inayofuata.

Mshambuliaji huyo anatumia mguu wa kushoto na anatarajiwa kuchukua nafasi aya Coutinho kama kocha huyo Mholanzi atamkubali.


Kabla ya kuja nchini, amewahi kuichezea klabu kongwe ya Tusinia ya Club African na ES Hammam-Sousse ingawa inaonyesha hakuwa akidumu katika kila klabu hata kwa msimu mmoja tu!

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply