SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / SAKATA MCHEZAJI ASIESTAHILI-REAL YATUPWA NJE COPA DEL REY!


REAL-CHERYSHEVReal Madrid imetupwa nje ya Kombe la Mfalme wa Spain, Copa del Rey, kwa kosa la kumchezesha Mchezaji asiestahili kwenye Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Timu 32 Jumatano Usiku waliyoifunga Cadiz FC 3-1.

Uamuzi huu umetolewa na RFEF, Shirikisho la Soka la Spain nan a kusambazwa na Kituo cha Radio cha Spain Cadena COPE.

HABARI ZA AWALI:
SAKATA MCHEZAJI ASIESTAHILI-REAL KUPIGANA ISITOLEWE COPA DEL REY!
RAIS wa wa Real Madrid Florentino Perez amelalamika kuwa wao hawana hatia na watapigana kupinga kutupwa nje ya Kombe la Mfalme, Copa del Rey, kwa kumchezesha Mchezaji asiestahili.

Jumatano Usiku, Real iliifunga Cadiz FC 3-1 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Timu 32 ya Copa del Rey na Bao lao la kwanza kufungwa na Winga kutoka Russia, Denis Cheryshev, ambae alipaswa kuwa Kifungoni kwa ajili ya Mechi hiyo baada ya kupata Kadi za Njano 3 Msimu uliokwisha kwenye Mashindano hayo akiichezea kwa Mkopo Villareal.

Baada ya Mashabiki kupiga kelele, wakiimba ‘’Benitez, Tizama Twitter!’, Real wakagundua kosa lao na kumbadili Cheryshev wakati wa Haftaimu kitu ambacho Kocha wa Real, Rafa Benitez, alikisema baada ya Mechi kuwa walikifanya kwa nia njema.

Hii si mara ya kwanza kwa Kocha wa Real Rafa Benitez kukumbwa na balaa kama hili kwani akiwa na Valencia Mwaka 2001 alichezesha Wachezaji Wanne kutoka Nchi ambazo si za Jumuia ya Ulaya wakati wanaruhusiwa Watatu tu walipocheza na Novelda na kushinda lakini wakatupwa nje ya Copa del Rey baada Novelda kukata Rufaa.

Mwezi Septemba Mwaka huu, Osasuna walitupwa nje ya Copa del Rey baada ya kumchezesha Mchezaji asiestahili walipocheza na Mirandes.

Rais Perez, akiongea na Wanahabari hapo Jana, amedai si Cheryshev wala Real waliojulishwa na Shirikisho la Soka la Spain, RFEF, kwamba Mchezaji huyo alipaswa kuwa Kifungoni kwa Mechi moja.

Nao Villareal wametupa Mpira kwa Real na kuwaambia kuwa wao hawana jukumu lolote na Mchezaji huyo kwa vile si wa kwao.

LA LIGA
Ratiba
Desemba 5
Real Madrid CF v Getafe CF
Granada CF v Atletico de Madrid
Valencia C.F v FC Barcelona
Deportivo La Coruna v Sevilla FC
Real Betis v Celta de Vigo

Desemba 6
Real Sociedad v SD Eibar
Villarreal CF v Rayo Vallecano
Sporting Gijon v Las Palmas

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply