Tajiri huyo anayetambulika kwa jina la Nassoro Ahmed bin Slum
anayemiliki kampuni ya Bin-slum Tyres Ltd, amejitokeza na kukiri
kumiliki baadhi ya makontena yaliyokumbwa na kashfa hiyo lakini amekana
kosa lenye sura ya kukwepa kodi akidai kuwa limefanywa na wakala wake.
“Wafanyabiashara hatuna mamlaka ya kulipa kodi moja kwa moja serikalini.
Tunalipa kodi kupitia kwa wakala aliyechaguliwa na serikali. Mimi
nilimlipa kazi wakala wangu ambaye nimekuwa nikifanya naye kazi kwa
miaka 10,” Bin Slum ameliambia gazeti la Raia Mwema.
“Mara kwa mara huwa ananiletea nyaraka za malipo ya kodi lakini
kwenye mzigo huu wa sasa ambao kontena zangu zina matatizo ya kodi,
alinitangulizia mzigo na mimi nikamdai nyaraka. Yeye aliniambia
ananiandalia faili,” alieleza.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliagiza wote wanaohusika na kashfa hiyo kukamatwa na kuchukuliwa hatua na kodi iliyokwepwa ilipwe.
Tayari watu 12 wanashikiliwa na jeshi la polisi kufuatia sakata hilo.
Home
/
MATUKIO
/
Tajiri Anayemiliki Makontena Yaliyopotea Bandarini Ajitokeza......Amtupia Lawama Wakala Wake
Tajiri Anayemiliki Makontena Yaliyopotea Bandarini Ajitokeza......Amtupia Lawama Wakala Wake
Tagged with: MATUKIO
Hakuna maoni :