SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / WAGOSI WA KAYA VS WANA KIMANUMANU HAKUNA MBABE, JKT YAWATUNDUA PRISONS 4-1


Watani wa jadi, Coastal Union 'Wagosi wa Kaya' na Afrika Sports 'Wana Kimanumanu' wamemaliza Tanga derby kwa kufungana bao 1-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, leo.

Mechi ilikuwa na mvutano mkubwa, lakini mwisho watani hao kila mmoja alikuwa na bao moja.

Juma Mahadhi ndiye aliyefunga bao la Coastal Union huku Mohammed Mtindi naye akiwafungia Wana Kimanumanu bao lao.

Wakati huo huo, JKT Ruvu wamewapa somo la “kijeshi” maafande wa Magereza Prisons kwa kuwachapa mabao 4-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara leo.

Mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, Samwel Kamuntu alifunga bao moja, Mussa Juma akatupia moja na Michael Aidan akifunga moja huku lile la Prisons likifungwa na Mohammed Mkopi.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply