HATIMAYE mmiliki wa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC), Moise Katumbi amekubali mshambuliaji wa
kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta kujiunga na KRC Genk ya Ligi Kuu
ya Ubelgiji.
Mchezaji huyo alitarajia kurejea jana nchini kwa ajili ya safari ya Ubelgiji kwenda kuanza maisha mapya katika soka la Ulaya.
Samatta tayari amekwishasaini mkataba wa awali na Genk wa miaka minne na sasa anakwenda kukamilisha taratibu zilizobaki.
Samatta na Genk wanataka kukimbizana na muda ili kuwahi kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili.
Meneja wa Samatta, Jamal Kisongo alisema kuwa hatimaye
Katumbi ameridhia Samatta aende klabu anayoipenda ili kuendeleza soka
lake.
Katumbi alikuwa anataka Samatta aende Nantes ya
Ufaransa, ili kucheza soka huko, lakini mchezaji huyo hakupenda kwenda
huko na alikuwa tayari kubaki Congo kumalizia mkataba wake unaomalizika
Aprili.
Hakuna maoni :