SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / CAVANI KUTUA OLD TRAFFORD.

CAVANIUPO UVUMI mzito huko Ulaya kuwa Fowadi wa Uruguay, Edinson Cavani, anaechezea Paris St Germain yuko mbioni kujiunga na Manchester United kabla Dirisha la Uhamisho halijafungwa mwishoni mwa Mwezi huu.

Hivi sasa ni Siri iliyo wazi kuwa Cavani hafurahii kabisa kuichezea PSG ambako Meneja Laurent Blanc humchezesha kama Winga badala ya Sentafowadi kama anavyopenda yeye binafsi.

Habari za Cavani kutua Man United pia zimeongezwa uzito na Madai ya Jarida la kuaminika kutoka huko Italy, Corriere Dello Sport, ambalo limedai Fowadi huyo wa zamani wa Napoli mwenye Miaka 28 atatua Old Trafford kwa Dau kubwa.
Msimu huu, Cavani amepachika Bao 10 katika Mechi 17 alizochezea PSG kwenye Ligi 1 huko France.

Kama ilivyo kawaida, Klabu ya Man United, ambayo bado haijanunua Mchezaji yeyote katika Dirisha la Uhamisho la Januari, haijazungumza lolote.

LIGI KUU ENGLAND
Ratiba
**Saa za Bongo            
Jumamosi 23 Januari 2016
1545 Norwich v Liverpool           
[Mechi kuanza Saa 12 Jioni]
Crystal Palace v Tottenham                  
Leicester v Stoke             
Man United v Southampton                  
Sunderland v Bournemouth                  
Watford v Newcastle                  
West Brom v Aston Villa             
2030 West Ham v Man City                  
Jumapili 24 Januari 2016
1630 Everton v Swansea            
1900 Arsenal v Chelsea

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply