SAFU ya Nusu Fainali za 2016 African Nations Championship (Chan 2016), ambazo ni Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wachezao ndani ya Afrika, Rwanda, Leo imekamilika baada ya Mali na Guinea kushinda Mechi zao za Robo Fainali.
Katika Mechi ya kwanza ya Robo Fainali iliyochezwa Stade Regional Nyamirambo, Mali iliyotoka nyuma kwa Bao 1 la Tunisia lililofungwa Dakika ya 14 na Mohamed Ali Monser, walizinduka na kupiga Bao 2 katika Dakika za 71 na 80 zilizofungwa na Aliou Dieng na kutinga Nusu Fainali ambako watacheza na Ivory Coast hapo Alhamisi.
Kwenye Mechi ya pili ya Robo Fainali iliyochezwa Umuganda Stadium, Guinea waliibuka kidedea kwa Matuta 5-4 dhidi ya Zambia kufuatia Sare ya 0-0 katika Dakika 120 za Mchezo.
CHAN 2016
ROBO FAINALI
Jumamosi Januari 30
Rwanda 1 Congo DR 2 [Congo DR 2 Rwanda 1 baada ya Dakika za Nyongeza 30]
Cameroun 0 Ivory Coast 0 [Ivory Coast 3 Cameroun 0 baada ya Dakika za Nyongeza 30]
Jumapili Januari 31
Tunisia 1 Mali 2
Zambia 0 Guinea 0 [0-0 baada ya Dakika za Nyongeza 30, Guinea wasonga Penati 5-4]
NUSU FAINALI
Jumatano Februari 3
Congo DR v Guinea
Alhamisi Februari 4
Mali v Ivory Coast
Jumapili Februari 7
Mshindi wa 3
FAINALI
Hakuna maoni :